Muungano wa Jubilee unaoongozwa na Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu, unadaiwa kuanza kulalamikia inachokiita mchezo mchafu unaochezwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Mgombea Mwenza wa Kenyatta katika kinyang’anyiro hicho, William Ruto, alitoa malalamiko hayo jana katika kituo kikuu cha kupokea na kutoa matangazo ya matokeo ya kura za urais, Bomas, jijini hapa, alipozungumza na waandishi wa habari.
Ruto alidai kuwa IEBC imeamua kuhesabu kura zilizoharibika pamoja na halali kwa shinikizo, ili kuunyima ushindi muungano huo katika raundi ya kwanza na akabainisha kwamba kama ikionekana ni muhimu, watashitaki mahakamani kupinga uamuzi huo wa Tume.
Ili mtu atangazwe mshindi katika uchaguzi wa Rais, ni lazima apate zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa au angalau asilimia 25 ya kura zilizopigwa katika majimbo 24. Kenya ina majimbo 47.
IEBC ilionesha kuwa kati ya matokeo yaliyokuwa yamefikishwa Bomas, kura 334,080 zilikuwa zimeharibika na kila baada ya muda mfupi idadi ilikuwa ikiongezeka.
Ilipofika saa 1.42 asubuhi, kura zilizoharibika zilikuwa 334,288, saa 2.11 asubuhi zikafika 334, 736.
Hadi 1.26 asubuhi jana, kura zilizokuwa zimeharibika zilikuwa ni nyingi kuliko jumla ya kura zote walizokuwa wamepata wagombea sita wa urais mbali na Uhuru na Raila Odinga.
Musalia Mudavadi alikuwa na kura 149,713, Peter Kenneth alikuwa na kura 31,189, Martha Karua kura 17,309, Profesa James ole Kiyiapi 17,700, Mohamed Abduba Dida 16, 262 na Paul Muite kura 5,548.
Juzi mchana, Mwenyekiti wa IEBC, Isaack Hassan, alisema kura zilizoharibika zitatumika kuhesabu idadi ya mwisho ya watu waliopiga kura, ili kupata matokeo ya urais.
Kwa maana hiyo, kama kura zilizoharibika zikijumuisha kupata idadi kamili ya kura zilizopigwa na kila mgombea kutoa kura halali alizopata, kuna uwezekano wa kurudia raundi ya pili, kutokana na uwezekano wa kukosekana kwa mgombea mwenye zaidi ya nusu ya kura zote.
“Kuna kura nyingi zimeharibika kuliko tulivyotarajia, kwa kweli ni jambo la kutupa wasiwasi kama Tume ni kwa nini kura zimeharibika!” Alishangaa Hassan juzi mchana, Bomas.
Alisema, baada ya kumalizika kwa mchakato wa uchaguzi, Tume itachunguza kubaini chanzo cha kuharibika kwa kura nyingi kiasi hicho.
“Hizi ni kura zilizopigwa na zimeharibika, labda kwa sababu zilipigwa isivyostahili,” alisema na kubainisha kuwa, baadhi ya kura ziliwekwa katika masanduku ya kura zingine.
“Rangi za kutambulisha masanduku hazikuwa nzuri kama ilivyostahili, ya kijani haikuwa imekolea, na labda ya bluu ingekuwa imekolea zaidi, labda rangi zingekuwa zimekolea zaidi,” alisema.
Alisema, huenda tatizo hilo lilisababishwa na kuongezeka kwa idadi ya kura zilizopigwa, kwa kuwa wapiga kura walipaswa kupiga kura sita ikiwamo ya kumchagua Rais, wawakilishi kwenye mabaraza ya kata, wabunge, wawakilishi wa wanawake bungeni, maseneta na magavana.
“Badala ya kuweka kwa Rais, labda wameweka kwa Gavana au mahali pengine…ama labda walikuwa wanaharibu wakati wanapiga kura,” alisema Hassan juzi mchana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Kura huharibika kama mpiga kura ameweka alama kwa zaidi ya mpiga kura mmoja, hivyo inakuwa vigumu kutambua alikuwa amemchagua yupi, na kama kura husika inawekwa kwenye sanduku lisilostahili.