Wachungaji watatu walikutana wasimuliane matatizo yao ili waweze kuombeana. Wa kwanza akasema: "Jamani mimi tatizo langu ni wizi. Yaani kila nikimaliza ibada lazima nidokoe sadaka." Wa Pili akasema: "Tatizo langu mimi ni uzinzi. Yani kila nikiona msichana lazima nimtongoze." Wa tatu akaanza kulia. Wenzake wakamuuliza kulikoni naye akawajibu: "Jamani mimi tatizo langu umbea, yani siwezi kabisa kutunza siri. Na haya yote lazima nikamweleze Askofu!" Kasheshe...
↧