Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

AJIZALISHA NA KUTUMBUKIZA KICHANGA KWENYE NDOO

$
0
0

Msichana mmoja mkazi wa Mtaa wa Zaire eneo la Kijenge Kaskazini mkoani Arusha, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru chini ya ulinzi mkali wa Polisi baada ya kujizalisha mwenyewe na kisha kumtumbukiza mtoto wake kwenye ndoo ya maji.

Baba mwenye nyumba ambayo binti huyo alikuwa amepanga chumba cha kuishi, Reuben Mollel alisema  msichana huyo alikuwa anajulikana kama ‘Dada Pendo,’  na kwamba  maisha yake hayakuwa wazi.
“Alipokuja kupanga hapa alidai kuwa yeye ni mwanafunzi, ila hivi karibunipia alionekana kuwa na mimba, hakuna kilichojulikana tena hadi jana, ambaponyumba hii ilizingirwa na wanakijiji ambao hatimaye waligundua kitotokinachodhaniwa kuwa ni chake, kikiwa kimezamishwa kichwa chini, kwenye ndooya maji,” alisema baba huyo mwenye nyumba.
Taarifa za uwezekano wa kuwepo mtoto mchanga ndani ya chumba cha DadaPendo, ziliibuliwa na mpangaji mwenzake,  Mama Martha Lucas, ambayealidai kuwa alisikia sauti ya mtoto mchanga akilia usiku kucha na baadaekutoweka majira ya asubuhi.
“Nilikwenda kumgongea Dada Pendo chumbani kwake, kutaka kujua hali ya mtoto aliyekuwa analia usiku na kwa kweli nilishangaa sana, alipojibu kuwa hajuilolote kuhusu mtoto wala vilio vilivyokuwa vinasikika usiku huo,” alisemaMama Lucas.
Hata hivyo, jirani huyo aliamua kutoa taarifa kwa wapangaji wenzake pamojana wakazi wengine wa Kimandolu, ambao walimuita Mjumbe wa Mtaa wa KijengeKaskazini, Gabriel Joseph na pamoja walianza msako wa kukitafuta kichangahicho, hii ikiwa ni pamoja na kujaribu kuvunja choo cha shimo cha nyumbahiyo, wakidhani kuwa mtoto alitupiwa humo.
Baada ya juhudi zao kuambulia patupu, mkazi mmoja wa eneo hilo, NelsonKweka, alihisi kuwa pengine chumba cha huyo dada hakikukaguliwa vizuri nandipo alipofunua mfuniko wa ndoo ya maji ya plastiki na kumkuta mtoto mdogowa kiume akiwa ametumbukizwa humo, na tayari alikuwa ameshakufa.
Hatimaye polisi walipewa taarifa, lakini mara walipofika kwenye eneo latukio, walimkuta dada mtuhumiwa naye akiwa katika hali mbaya kiafya, penginekutokana na juhudi za kujizalisha mwenyewe usiku.
Dada Pendo alikimbizwa hospitalini Mount Meru, huku mtoto wakeukipelekwa kuhifadhiwa katika nyumba ya maiti hospitalini hapo.
Ofisa Habari wa Polisi mkoani hapa, Rashid Nchimbi alisema polisi wanasubiri afya ya dada huyo itengemae ili aweze kulisaidia jeshi hilo katika uchunguzi zaidi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles