![]() |
Bwalo la Riva Bingo, mjini Sutton. |
Mcheza kamari ya bingo mwenye umri wa miaka 80 amekamatwa kwa madai ya kumshindilia konde mstaafu mwingine usoni.
Wanawake hao wawili waligombana kwenye Bwalo la Riva Bingo, mjini Sutton, kusini mwa London, wakati wakiwa kwenye foleni ya chakula cha mchana Jumapili iliyopita, kwa mujibu wa polisi.
Mwanamke mwenye umri mdogo, miaka 72, alimtaka yule mwenye umri mkubwa aharakishe na kumwita 'mwanamke mzee mpumbavu', ilidaiwa.
Mwanamke mwenye umri mkubwa alijibu mapigo kwa hasira dhidi ya mwenzake, na kumporomoshea 'matusi mazito', kwa mujibu wa polisi.
Kama haikutosha, mwanamke huyo mwenye miaka 80 akamrushia konde usoni mwenzake mdogo. Mwanamke huyo wa miaka 72 alipata michubuko kidogo.
Wakati huo, wafanyakazi walikuwa wakigawa chakula cha mchana kwenye bwalo hilo la kamari mjini Sutton.
Msemaji mmoja wa polisi mjini Sutton alisema: "Maofisa kutoka katikati ya mji wa Sutton walimuonya mwanamke huyo mwenye miaka 80 kabla ya kuhojiwa nyumbani kwake.
"Polisi kwa sasa wameamua kutochukua hatua zozote zaidi kuhusiana na suala hili."
Msemaji wa Bwalo la Riva Bingo Sutton hakuweza kupatikana.