Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4621

AMUUA KAKA YAKE KWA KUMKATA NA SHOKA...

$
0
0
Mkazi wa kijiji cha Fyengelezya, Manispaa ya Sumbawanga, Didas Choma (35), ameuawa kikatili na mdogo wake wa tumbo moja, Frank Choma (30), kwa kumkata kichwa kwa shoka kutokana na mgogoro wa shamba la urithi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda,  amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo  ya kikatili kijijini Fyengelezya, Machi 2 mwaka huu  saa 3.00 usiku  karibu na nyumba  ya marehemu.
Kwa mujibu wa Mwaruanda, uchunguzi wa  awali umebainisha kuwa chanzo  cha mauaji hayo ni mgogoro wa shamba la urithi, ambapo mtuhumiwa anadai  marehemu na mama yao mzazi, waliuza shamba hilo  kisha kugawana  fedha  peke yao bila ya kumshirikisha.
Akisimulia mkasa  huo, Kamanda Mwaruanda  amedai kuwa  usiku huo wa tukio  hilo, mtuhumiwa  alijificha karibu na nyumba ya kaka yake  huyo  akiwa na shoka, akimsubiri arejee nyumbani kwake akitokea matembezini.
Inadaiwa Frank  alimshtukiza kaka yake  na kumkata kwa shoka kichawani  hadi  alipohakikisha kuwa amefariki ndipo  akatoroka na kujificha kusikofahamika ambapo  polisi wilayani Sumbawanga bado  inamsaka.
Baadhi ya  ndugu wa marehemu wakizungumza kwa  nyakati tofauti na mwandishi, kwa masharti ya majina  yao kutoaandikwa gazetini, wamethibitisha  kuwa shamba  hilo  lililozua mgogoro kwa wanafamilia  hao, liliachwa  na baba  mzazi  wa vijana  hao.
Pia wamethibitisha  kuwa  maziko  ya  ndugu yao  yalifanyika kijijini  hapo  juzi saa 12.00 jioni.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4621

Trending Articles