Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

KESI YA 'WATOTO WA MBWA' YAAHIRISHWA

$
0
0
Kesi inayowakabili vijana saba wanaojiita ‘watoto wa mbwa’, imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu, kutokana na hakimu anayesikiliza shauri hilo, kutokuwepo mahakamani.
Akiahirisha shauri hilo juzi, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Tharasira Kisoka alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa tarehe hiyo, kwani Hakimu Wilberforce Luhwago ambaye anasikiliza shauri hilo, hayupo.
Kesi hiyo imefikia hatua ya kusikilizwa, kutokana na upelelezi wa shauri hilo, kukamilika. Watu hao walirudishwa rumande kutokana na shauri hilo halina dhamana.
Washitakiwa hao ni Sijah Abdallah (19), Sadick Chitemo (25), Shaibu  (30), Balozi Inasio (19), Zagomba Kihongo (20), Isack Lukosi (17) na Hatibu Rajabu (24), wote wakazi wa Kiwalani Dar es Salaam.
Watu hao walidaiwa kuwa Januari mosi mwaka huu, maeneo ya Yombo Kiwalani wilayani Ilala, waliiba Sh 150,000 na  simu ya mkononi aina ya Nokia, mali ya Suma Fungo. Ilidaiwa  kuwa kabla ya tukio hilo walimpiga mlalamikaji kwa mapanga na visu ili kuchukua vitu hivyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

Trending Articles