Zaidi ya watoto 37 kati ya 100 walio na umri chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Dar es Salaam, wana upungufu wa Vitamini A.
Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadiki alisema hayo wakati akizungumzia utoaji wa matone ya Vitamini A na dawa za minyoo kwa watoto wenye miezi sita hadi 59.
"Katika nchi yetu upungufu wa vitamini A ni tatizo sugu sana, hasa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano, ambapo takwimu zinaonesha watoto 33 kati ya 100 nchini wana upungufu wa vitamini A," alisema.
Alisema vitamini A inahitajika mwilini ili kusaidia ukuaji wa mwili na akili, kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na kuimarisha uwezo wa macho kuona vizuri.
"Uhitaji wa vitamini A kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano ni mkubwa zaidi na kwa umuhimu wake serikali imeendelea kuratibu utoaji wa dawa hizo," alisema.
Sadiki alisema mkoa huo, umeendelea kutoa dawa hizo katika Manispaa zake tatu, wakiwa na lengo la kufikia zaidi ya asilimia 80 kwa watoto wote wenye umri husika, lakini kwa bahati mbaya hawajaweza kufikia lengo hilo.
"Utafiti uliofanyika Januari mwaka huu, unaonesha kwamba mkoa wetu umefikia asilimia 37 ya watoto wote waliolengwa, hivyo hatufanyi vizuri katika hili na kama tutaendelea hivi hatutafikia malengo ya taifa," alisema.
Alisema katika mkoa huo, utoaji matone hayo na dawa za minyoo, ulianza Julai 7, mwaka huu na utaendelea hadi Julai 30.