Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Julai 29 mwaka huu kuendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi ya kukutwa na bomu bila kibali, inayowakabili watu wanne.
Washitakiwa katika kesi hiyo ni Fadhil Kitogo, Idd Muhina, Shukuru Kitogo na Julius Chonya.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo, Julai 30, mwaka jana, katika eneo la Vingunguti Becco, Dar es Salaam.
Kitogo na washitakiwa wenzake wanaodaiwa kukutwa na bomu la kutupa kwa mkono bila ya kuwa na leseni, walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Agosti, 2013.
Washitakiwa wapo rumande kwa kuwa mashitaka yanayowakabili hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.