Kikosi cha Zimamoto na uokoaji nchini, kimenunua vifaa 100 vitakavyosaidia kuzima moto bila kutumia maji vyenye thamani ya Sh milioni 200.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akipokea vifaa hivyo, Kamishna Msaidizi wa Zimamoto, Jesuald Ikonko alisema vifaa hivyo vimenunuliwa kutoka kampuni ya Dry Sprinker Powder Aerosol (DSPA5) ya Uholanzi.
“Leo tumepokea vifaa 25 ambayo ni awamu ya kwanza kwani vifaa vilivyoagizwa na Serikali ni 100,” alisema Ikonko.
Alisema vifaa hivyo ni kinga kwa mazingira na vinasaidia kupunguza hasara inayotokea wakati moto ukitokea kwani vifaa hivyo vina uwezo wa kuzima moto kwa haraka.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Your Solution Tanzania, Damian George ambaye ndiye aliyekabidhi vifaa hivyo, alisema vifaa hivyo vinatumika kuzima moto wa nyumba kubwa na majengo na havitumiki kuzima moto unaounguza magari au unaowaka nje.
Alisema pamoja na vifaa hivyo kuandaliwa na kutumika sawa na bomu, lakini hakilipuki kama bomu na haiongezi presha kwenye eneo la tukio kwa maana ya kuleta mtikisiko.
“Kifaa hiki kinazima moto kwa haraka bila wewe kuingia ndani ya chumba au eneo la moto na kuzuia hasara kubwa inayoweza kusababishwa na moto,” alisema George.
Aliongeza kuwa DSPA5 haiharibu hewa ya oksijeni wala kuichukua na kuichafua bali ni rafiki kwa mazingira na mimea na haina madhara kwa maisha ya binadamu na wanyama.