Chama cha Wananchi ( CUF) kinatarajia kuanza kufanya mikutano ya hadhara ya kuhamasisha shughuli za chama hicho mkoani Mtwara mara baada ya mfungo mtukufu wa Ramadhani.
Hatua hiyo, ya CUF itakuwa ni kinyume na katazo la Jeshi la Polisi nchini, ambalo lilipiga marufuku mikutano yoyote ya kisiasa mkoani humo, kutokana na vurugu zilizoibuka kuhusu gesi.
Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Abdul Kambaya, pamoja na kwamba jeshi hilo limezuia kufanya mikutano mkoani humo, bado vyama vingine vimekuwa vikiruhusiwa kufanya mikutano hiyo bila tatizo.
“Katazo hili halina mashiko kwa vile limekuwa likiruhusu CCM wafanye mikutano huku wapinzani wakizuiwa,” alisema Kambaya.
Alisema Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho, uliofanyika mwezi Juni, mwaka huu, ulilaani kizuizi hicho kilichowekwa na Polisi kwa vyama vya upinzani, huku likitoa fursa kwa CCM kufanya mikutano hiyo na kulindwa na jeshi hilo.
“Katazo hili limekuwa ni kinyume na demokrasia nchini kwani kwa muda mrefu limefanya wananchi wa Mtwara wasijumuike kujadili mustakabali wa maisha yao,” alisema.
Mnamo Mei, mwaka jana jeshi hilo la Polisi, lilipiga marufuku mikutano yoyote ya kisiasa mkoani Mtwara kutokana na hali ya vurugu zitokanazo na gesi zilizojitokeza mkoani humo.