Kampuni ya Vita Foam Tanzania Limited imepata cheti cha uthibitisho pamoja na alama za ubora wa kimataifa kutokana na kutimiza viwango vya usimamizi wa ubora vinavyotambulika kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikabidhiwa vyeti hivyo jijini hapa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Suraj Chandalia alisema bidhaa za kampuni hiyo sasa zitakuwa na alama za ubora wa bidhaa (bar code) na hii itasaidia bidhaa zake zitambulike katika maduka makubwa.
Alisema kampuni hiyo imekuwa kampuni pekee ya magodoro nchini ambayo imefikia uthibitisho wa Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) 9001:2008 ambayo imefanyiwa tathmini na kupitishwa na Bodi Maalumu ya Uthibitisho Kimataifa.
“Pamoja na cheti cha uthibitisho na Bar code, Vita Foam itaendelea kuelekeza nguvu zake kwa kutimiza mahitaji ya wateja na matarajio kuhakikisha bidhaa zinahusishwa daima na ubora,” alisema Chandalia.
Mwakilishi wa ISO nchini, Boniface Kanemba wakati wa kukabidhi cheti hicho alisema amefurahishwa kuona kampuni ya magodoro kuwa ya kwanza kupata cheti cha ubora wa kimataifa.
“Nawasifu sana Vita Foam ila wanatakiwa kujituma na kuongeza juhudi katika uzalishaji wa bidhaa bora kwani kupata cheti ni kazi moja ila kulinda cheti ni kitu kingine,” alisema Kanemba.
Meneja Masoko Chama cha Wafanyabiashara kinachoundwa na wazalishaji, wasafirishaji, wauzaji na wanunuzi nchini (GS1), Esta Budili wakati akikabidhi cheti cha ubora wa bidhaa kutoka GS1 Tanzania National alisema wafanyabiashara wanatakiwa kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo zitawasaidia kupata alama za ubora wa bidhaa ambayo itawasaidia katika upatikanaji wa masoko.