Rais Jakaya Kikwete amezitaka taasisi za dini, kuendelea kuiombea Serikali, vyama vya siasa na mchakato wa Katiba mpya ili taifa liweze kupata Katiba mpya na bora kwa amani.
Alitoa wito huo wakati akihutubia maelfu ya wananchi kwenye kilele cha Sherehe za Miaka 75 ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG). Sherehe hizo zilifanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya jana.
Rais alisema ni vyema taasisi za dini nchini, kuombea Serikali, vyama vya siasa na mchakato wa katiba unaoendelea ili kuwezesha kupata Katiba bora na nzuri kwa njia ya amani na utulivu.
Akijibu ombi la Rais Kikwete, Askofu Mkuu wa TAG, Dk Barnabas Mtokambali, alisema Kanisa la TAG limekuwa likifunga na kusali na litaendelea kufanya hivyo mpaka nchi itakapopata Katiba mpya na nzuri kwa amani na utulivu.
“Wote tumekuwa na kazi moja, ambayo ni kuongoza na kuwatumikia watu wa Mungu kama wachungaji wa kiroho. Na kupitia sisi wote tunapata mafanikio tuliyokusudia,” alisema Mtokambali.
Mchakato wa Katiba mpya ulianza kuundwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo baadaye ilikusanya maoni ya wananchi katika mikoa yote nchini. Baada ya hapo, Tume hiyo iliyoongozwa na Jaji mstaafu Joseph Warioba, ilitayarisha rasimu ya kwanza ya Katiba na kuikabidhi serikalini.
Kisha, tume hiyo ilitayarisha rasimu ya pili na kuikabidhi Serikali mwaka jana mwishoni. Hatua iliyofuata ni kuundwa kwa Bunge Maalum la Katiba, ambalo lilikutana huko Dodoma kwa mara ya kwanza kwa miezi miwili. Baadaye bunge hilo, liliahirishwa hadi Agosti 5, mwaka huu, litakapoendelea tena.
Kikwete alisema kumekuwepo na ongezeko la teknolojia mpya, mfano matumizi ya intaneti na vituo vya televisheni, katika kueneza neno la Mungu. Lakini, pamoja na ongezeko hilo la neno la Mungu, inasikitisha kuona kuwa maovu bado yanaongezeka.
“Magereza yamejaa wahalifu, baadhi yao ni viongozi wa dini, watu ambao wanatarajiwa kusaidia taifa kuhubiri neno la Mungu kwa kujenga maadili kwa watu wake. Hali imebadilika sana, ni wakati ambao tunatakiwa kuiangalia jamii yetu kwa mtazamo tofauti. Tunahitaji ushiriki kutoka vyama vyote na madhehebu ya kupunguza maovu,” alisema.
Kikwete alisema chini ya mwavuli wa dini, maovu mengi yamekuwa yakifanyika, jambo ambalo linatakiwa kuachwa mara moja. Alisema jambo hilo likiachwa, watu watarejesha imani kwa dini, kuwa ni sehemu ya kwenda kupata msaada na sio kukimbiwa.
Alisema viongozi wa dini, wana nafasi ya pekee, kutokana na watu kuwaheshimu na kusikiliza kile wanachosema, tofauti na viongozi wa Serikali.
Rais alisisitiza kuwa maendeleo ya nchi, yanategemea viongozi wa dini kuwa makini na kutimiza majukumu yao.
Katika maadhimisho hayo, Kikwete alizindua kitabu kinachoelezea Historia ya Kanisa la TAG. Pia alitoa medali na tuzo kwa watu ambao wamekuwa viongozi wa Kanisa katika miaka 75, akiwamo Mkuu wa Baraza la Kanisa la Assemblies of God la Marekani. Kanisa hilo pia lilimkabidhi Rais Kikwete tuzo. Tuzo hiyo ilitolewa na Askofu Mkuu wa TAG, Dk Mtokambali.
Akizungumzia maadhimisho hayo, ambayo yalipambwa na watoto kufanya maonesho mbalimbali, Dk Mtokambali alisema sherehe hizo ni shukrani kwa Mwenyezi Mungu, ambaye amekuwa nguzo ya wao kufikia mafanikio hayo.
Mtokambali alisema katika miaka 75 ya kutoa huduma nchini, kanisa hilo limeweza kujenga zaidi ya shule 20.
Pia, alisema kanisa hilo lina mpango wa kujenga vyuo vikuu viwili katika mikoa ya Iringa na Kilimanjaro na miradi ya visima huko Dodoma, Singida, Same na Manyara.