Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4673

WAZIRI KUTEMBELEA ASASI ZA KISHERIA DAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki anafanya ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia leo katika Jiji la Dar es Salaam kutembelea asasi zinazotoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi.
Lengo la ziara hiyo ni kuona huduma zinazotolewa na asasi hizo ikiwa ni pamoja na kukutana na wananchi wanaopata huduma hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na  Wizara hiyo jana, Pamoja na kujionea huduma hizo, Naibu Waziri anatarajiwa kukagua ufanisi wa kazi zinazofanywa na asasi hizo pamoja na changamoto zinazowakabili.
Pia atapokea maoni, ushauri na kubadilishana mawazo na wadau ili kujua jinsi ambavyo Serikali inaweza kuboresha utoaji wa huduma hii.
Katika ziara hiyo, Kairuki atatembelea jumla ya asasi 13 ikiwa ni pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Taasisi ya Haki za Binadamu na Mazingira (Envirocare), Kamati ya Msaada wa Kisheria ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo.
Nyingine ni pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC) na Kituo Kinachoshughulikia Maslahi ya Wanawake na Watoto (TWCWC).
Taasisi nyingine atakazotembelea ni Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wajane na Watoto (CWCA), Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Kituo cha Msaada wa Kisheria cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Nyumba ya Amani na Ofisi ya Mfuko wa Huduma za Kisheria (Legal Services Facility).
Kairuki atamaliza ziara yake kwa kutembelea Sekretariati ya Msaada wa Kisheria Tanzania inayoratibu shughuli za utoaji wa Msaada wa Kisheria Tanzania na kisha
kufanya mkutano wa majumuisho na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4673

Latest Images

Trending Articles