Rais Jakaya Kikwete ameziagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya kulipatia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) bila gharama ili liweze kutekeleza mradi wake wa ujenzi wa nyumba bora za bei nafuu.
Alitoa agizo hilo jana katika kijiji cha Kasera kilichopo kata ya Parungu wilayani Mkinga alipofungua mradi wa ujenzi wa Nyumba Bora 40 za gharama nafuu zilizojengwa na NHC ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga.
Katika mradi huo wa nyumba za bei nafuu Mkinga, halmashauri imechangia ardhi na unatarajiwa kugharimu kiasi cha Sh bilioni 1.4 hadi kukamilika, fedha ambazo zinajumuisha ujenzi wa makazi yenye vyumba viwili na vyumba vitatu pamoja na zahanati, shule ya chekechea na maduka ya bidhaa za aina mbalimbali.
“Nachukua nafasi hii kuwapongeza NHC kwa kujenga nyumba hizi za bei nafuu ambazo sisi serikali tunazihitaji sana ili kuwawezesha wananchi wetu kuishi kwenye makazi bora…mwito wangu kwa kila halmashauri sasa ni kuhakikisha inatenga ardhi ya kutosha na kulipatia shirika kwa bila gharama yoyote kwa ajili ya kukamilisha azma yake hii”, alisema.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Felix Maagi alisema lengo la kubuniwa kwa mradi huo ni kupunguza tatizo la uhaba wa nyumba hususan za watu wa kipato cha kati na chini katika maeneo mbalimbali nchini na kuwawezesha watumishi kuishi karibu na vituo vyao vya kazi ili kuwaondolea gharama za usafiri.
“Ni ukweli ulio wazi kwamba hapa nchini kuna mahitaji makubwa ya nyumba yanayokadiriwa kufikia milioni tatu hivi sasa yakiongezeka kwa idadi ya nyumba 200,000 kila mwaka wakati uzalishaji wa nyumba ni kiasi cha asilimia 10 ya mahitaji ya mwaka mzima,” alisema na kuogneza:
“Kwa kuwa ujenzi wa mradi huu unahitaji ardhi ya kutosha changamoto inayotukabili ni halmashauri nyingi kutokuwa na mpango mahususi wa maendeleo ya ardhi na hivyo kusababisha NHC kulazimika kununua ardhi kwa fedha ya mikopo ya benki ili kulipa fidia hatua ambayo inaongeza bei ya nyumba hizo zinazoendelea kujengwa katika halmashauri mbalimbali”.
Maagi alisema nyumba hizo zitauzwa kwa bei ya kati ya Sh milioni 34 na 40 bila kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kwamba nyumba kama hizo pia zimejengwa katika maeneo mengine 14 ya halmashauri za miji na wilaya ambazo zitawapatia makazi bora wananchi wapatao 7,285 pamoja na ajira za moja kwa moja 7,170.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete pia amezindua nyumba tano za makazi bora ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mkinga zilizogharimu zaidi ya Sh milioni 340 kupitia Mfuko wa serikali za mitaa na kuwataka watumishi hao kuacha tabia ya kupenda kuishi nje ya eneo lao la kazi.