Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4658
↧

TACAIDS WAFAFANUA DAWA YA KUFUBAZA VIRUSI VYA UKIMWI

$
0
0
Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imethibitisha kwamba dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi  (ARVs) zinapatikana na zenye ubora zaidi tofauti na taarifa za baadhi ya vyombo vya habari kueleza kuwa dawa hizo hazipatikani.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS, Dk Fatma Mrisho wakati alipozungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano na wadau wa Ukimwi wa kujadili matumizi sahihi ya rasilimali za mapambano dhidi ya Ukimwi.
Alisema Serikali kupitia ngazi za juu imekuwa ikichukua jitihada mbalimbali kuhakikisha ARVs zinapatikana na kuanzia Januari na Februari mwaka huu, iliagiza dawa hizo kutoka kwa watengenezaji nje ya nchi.
Hata hivyo, alisema kuna kipindi kifupi dawa hizo zilichelewa kufika kutoka sehemu zinakotengenezwa ingawa Serikali ilifanya juhudi za haraka kuhakikisha dawa hizo zinapatikana.
Akizungumzia mkutano huo wa siku moja, Dk Mrisho alisema wadau wa Ukimwi wa Tanzania na nje wanaangalia iwapo rasilimali za Ukimwi zinatumika kwenye mahitaji makubwa zaidi na zinatumika kwa ufanisi kama inavyotakiwa.
Aliongeza kuwa watajadili matumizi ya fedha za kufadhili mapambano dhidi ya Ukimwi  ambazo zinaendelea kupungua ili kuhakikisha fedha wanazopata zinatumika kwenye maeneo muhimu katika masuala ya Ukimwi.
Alisema mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Ukimwi Ulimwenguni kutokana na wahisani kupunguza misaada ya kifedha katika mapambano dhidi ya Ukimwi kutokana na mtikisiko wa fedha duniani.
↧

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4658

Latest Images

Trending Articles