Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

MAHUJAJI WANAOENDA KUHIJI MAKKA WAONYWA

$
0
0
Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania(TAHAFE) limewatahadharisha  waumini wote wa dini ya Kiislamu, wanaotarajia kwenda katika Ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia, kuwa makini na matapeli.
Matapeli hao ni wale wanaotumia kigezo cha kuratibu safari ya kwenda nchini humo, kwa lengo la kujipatia fedha.
Hayo yalisemwa  Jijini Dar es Salaam  jana na Katibu wa TAHAFE, Swed Swed wakati  akizungumzia maandalizi ya safari ya kwenda Hijja, inayotarajiwa kufanyika baada ya Mfungo wa Mwezi  Mtukufu wa Ramadhan.
Swed alisema kumekuwepo na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiojulikana dhidi ya waumini wa dini hiyo, wanaotaka kwenda katika miji ya Madina na Macca kwa ajili ya kuhiji.
Alisema hatua  hiyo imekuwa ikisababisha usumbufu kwa mahujaji pamoja na taasisi hiyo.
“Baadhi ya matapeli hao wamekwenda mbali na kutumia majina ya wamiliki wa Kampuni za Bakhresa na Oilcom, kwamba wametoa msaada wa kuwasafirisha waumini wenye nia hiyo ya kwenda kuhiji na kuwataka wao kuchangia kiasi kidogo kwa ajili ya kupata hati zao za kusafiria.
“Tunawaomba Waislamu wote wenye malengo ya kwenda  katika ibada hiyo, kuwa makini na matapeli hao na kufuata taratibu za uhakika, zinazotolewa na taasisi kumi na tatu zilizokidhi vigezo vya kuwasafirisha mahujaji hao
kwenda katika ibada hiyo,” alisema Swed.
Alitaja taasisi hizo kuwa ni Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Tanzania Muslim Hajj Trust, Zam Zam Centre, Khidmat Islamiya Chartable Society, Al-Bir Hajj Group, Tanzania Charitable Development Organisation, Taibah Hajj and Umrah na Amaan Travel.
Zingine ni Jamarat Hajj and Umrah Traveller, Al-Bushra Tours, Masjid Adl, Al-Jazira International Hajj Trust na Peace Travel and Tours.
Alisema jumla ya taasisi 23 zimepewa ridhaa ya kusafirisha mahujaji hao, kwenda nchini Saudi Arabia. Lakini, kutokana na baadhi ya taasisi hizo kushindwa kukidhi matakwa yaliyowekwa, taasisi kumi hazitoweza kuwasafirisha mahujaji hao labda kwa kushirikiana na taasisi zilizokidhi vigezo hivyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

Trending Articles