Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

DAWASA YAPANUA MTAMBO RUVU JUU, YAJENGA CHUJIO

$
0
0
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka  Dar es Salaam imeanza  upanuzi  mkubwa wa mtambo wa Ruvu Juu, ikiwemo kujenga chujio mpya.
Upanuzi wa mtambo huo utakapokamilika, utaongeza uzalishaji  kutoka lita milioni 82 za maji kwa siku hadi lita milioni 196.
Kazi hiyo itaenda  sambamba na ulazaji wa bomba kubwa la kusafirisha maji kutoka  mtambo wa Ruvu Juu hadi Kibamba na kisha Kimara.
Hayo yalibainika wakati wa ziara ya kawaida ya  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Dk Eve-Hawa Sinare. Katika ziara hiyo ya juzi ya kukagua miradi ya DAWASA, Dk Sinare alifuatana na  Mwenyekiti wa Kamati  ya Ufundi ya mamlaka hiyo, Christine Kilindu na Meneja wa Miradi, Romanus Mwang’ingo.
 Mwang’ingo alimweleza Dk Sinare kuwa kazi ya kupanua mtambo, inafanywa na kampuni ya Va Tech Wabag kutoka India na tayari mkandarasi ameanza kazi ya ujenzi wa chujio mpya ya maji. Dk Sinare alimshuhudia mkandarasi huyo akiendelea na kazi huko Mlandizi.
“Kazi itakamilika baada ya miezi 18. Mradi ulianza mwezi  Februari mwaka huu na matarajio ni kumalizika mwezi Agosti mwaka 2015. Mradi utagharimu shilingi bilioni 65.11,” alisema.
Kuhusu ulazaji wa bomba kubwa, Mwang’ingo alisema mkandarasi amekamilisha upimaji (survey) wa njia ya kupitisha bomba hilo na ameanza kutengeneza mabomba hayo huko India, kama mkataba unavyosema. Pia, mkandarasi huyo ameanza kujenga  ofisi ya mradi mjini Kibaha. Dk Sinare alishuhudia pia ujenzi huo ukiendelea.
Bomba hilo kubwa litajengwa chini ya njia ya umeme  wa Gridi ya Taifa kutoka Ruvu Juu huko Mlandizi hadi Dar es Salaam. DAWASA imeshakubaliana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhusu kutumia njia hiyo ya Tanesco.
“Katika mradi huu wa Ruvu Juu, tutaweka bomba kubwa chini ya njia kuu ya umeme ili kuepuka matatizo tuliyoyaona katika mradi wa Ruvu Chini, ambako watu kadhaa wamekataa bomba kubwa lisipitishwe katika baadhi ya maeneo  ” alisema.
Kazi zitazohusika katika mradi huo wa Ruvu Juu ni: Ujenzi wa bomba jipya kutoka  Ruvu Juu hadi Kibamba, lenye kipenyo cha milimita 1200 na urefu wa kilometa 40, ujenzi wa tangi jipya Kibamba lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 10 na ujenzi wa matangi mawili huko Kimara. Mradi ulianza Machi mwaka huu na utakamilika  mwezi Septemba mwakani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles