Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jana imezindua utumiaji mitandao katika utoaji wa leseni ya biashara.
Meya wa Manispaa hiyo, Jerry Silaa, alizindua mtandao huo jana katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema mtandao huo wa http:ilala.kpk.fi/ebusiness utawezesha wafanyabishara katika manispaa hiyo kujaza fomu kwa ajili ya kupata leseni.
“Manispaa yetu inakuwa ya kwanza katika kila jambo la kujiongezea kipato hivyo ninawaalika Manispaa nyingine kuja kujifunza kutoka kwetu kwa nia ya kuongeza kipato,” alisema.
Alisema utoaji huo wa leseni umeunganishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wenye kuonesha taarifa zote za namba ya mlipa kodi (TIN) inayowatambulisha wafanyabiashara wote na kuonesha taarifa zao sahihi.
Alisema kutokana na kuungana huko iwapo mfanyabiashara ataandika taarifa ambazo si sahihi, mtandao utamkatalia hivyo kusaidia kuondokana na udanganyifu.
Silaa alisema leseni inayotolewa kwa mtandao wa kompyuta inaweza kuhakikiwa kwa kutumia simu za mkononi ambapo kwa watatumia sehemu iliyoandikwa GR Code kupata taarifa sahihi.
Alisema kwa kutumia njia hii itasaidia kuongeza kipato na pia kuweka ukaguzi kwa wafanyabiashara huku wakiwa na mipango ya kutumia mitandao katika kutoa leseni za viwanja na majengo hivyo kuondoa misongamano ya watu.
Meya alisema pia utoaji leseni hizo kwa mitandao itasaidia katika kukabiliana na utoaji wa leseni feki pamoja na kuwadhibiti vishoka wanaowadanganya wafanyabiashara katika Manispaa hiyo.