Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA YAKABIDHIWA RUNGU

$
0
0
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Fakhi Jundu amesema kuanzia sasa watumishi wote wa mahakama wataajiriwa kupitia Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Hatua hiyo imefikiwa kuondoa malalamiko  ya wafanyakazi wengine wa mahakama wasio majaji na mahakimu.
Ilielezwa kwamba wafanya kazi hao walikuwa wakiajiriwa na Serikali kuu,  hali iliyokuwa ikisababisha kutonufaika na uboreshwaji wa maslahi unaofanywa na mahakama.
Jaji Jundu alisema hayo  baada ya kutembelea banda la Mahakama katika maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara, Dar es Salaam yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema hatua hiyo ni sehemu ya maboresho ya idara ya mahakama kuwahudumia wananchi ipasavyo na kuondoa malalamiko.
Alisema malengo ni kwamba, baada ya miaka michache ijayo,  shauri likipelekwa mahakamani  linashughulikiwa si zaidi ya siku moja baada ya kufunguliwa.
“Katika maboresho hayo pia tunaangalia utendaji kazi kwa lengo la kubadilisha utendaji kazi na ufanisi wa mahakama kwa kila mtendaji kumpatia takwimu za utendaji kazi pamoja na vigezo maalum,” alisema Jaji Kiongozi.
Alisema kwa majaji na mahakimu wangepangiwa kusikiliza mashauri 220 kwa mwaka kila mmoja katika kila kanda huku wakiendelea kutoa vigezo kwa wasajili na watendaji wengine.
Alisema lengo kubwa ni kila mmoja kufanya kazi yake ipasavyo huku wakiboresha maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwa na mtendaji mkuu wa Mahakama, kuanzisha  mfuko wa mahakama na kuwa na  idara mpya ya ukaguzi na usimamizi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles