Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

KKKT KUANZISHA MFUKO WA MAFAO KWA WATUMISHI WAKE

$
0
0
Kanisa  la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodomainakusudia kuanzisha  mfuko kutoa mafao  maalumu kwa  Watumishi  wake baada ya kustaafu kazini.Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Dodoma, Robert Mgaya alisema hayo jana wakati wa mahojiano na wanahabari juu ya kuanzishwa kwa mfuko huo.Alisema Halmashauri Kuu ya Dayosisi hiyo ilikaa  Juni 12, mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake Askofu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu  na kukubaliana kupitisha mpango huo wa kuwasaidia watumishi hao baada ya kustaafu.Mgaya alisema  sababu ya kuanzisha mfuko huo ni  baada ya kuona watumishi wa kanisa hilo  wanapostaafu maisha yao na familia zao kukosa mwelekeo na kuyumba kiasi cha  kusikitisha.Alisema  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Dayosisi hiyo  walitafakari kwa makini na kuona kuwa watumishi hao walilitumikia Kanisa kwa uaminifu, upendo na  nguvu zao zote  lakini mwisho  wa siku hakuna anayewajali na kuishi maisha kama wakimbizi.Mgaya alisema Halmashauri Kuu ilikubaliana kuwepo na Jumapili moja kila mwezi  kwa sharika zote na Mitaa ya Dayosisi hiyo kutoa sadaka maalumu kwa ajili ya mfuko huo kwa kiwango  walichopangiwa.Aidha alisema katika kuhakikisha kuwa wamekusudia kuhusu kuanzisha mpango huo  makanisa yote Julai 13, mwaka huu wataanza kufanya mchango  maalumu kwa ajili ya kuzindua mfuko huo rasmi.Alisema Jumapili iliyopita wachungaji wote wa kanisa hilo walibadilishana vituo  vyao vya kazi ili kuwahamasisha Wakristo wa makanisa yao juu ya kujiandaa kuanza kutoa michango ya kuanzisha mfuko  huo.Mgaya alisema Kanisa lilikuwa likiwalipia watumishi wao katika mifuko ya kijamii lakini kutokana na mishahara yao kuwa midogo fedha hizo hazikidhi mahitaji yao  baada ya kustaafu kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kifamilia zao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

Trending Articles