Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

MAJAMBAZI WALIOUA SISTA KATOLIKI WATIWA MBARONI

$
0
0
Jeshi la Polisi kanda ya Dar es salaam limewakamata majambazi  sugu nane  ambao wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ya ujambazi na wawili kati wamehusishwa na tukio la kuuwawa kwa mtawa lililotokea jijini Dr es salaam.
Hayo yalisemwa jana na Kamishna wa polisi kanda maalum Dar es salaam Suleiman Kova wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema katika uhalifu huo majambazi hao walisababisha vifo,majeraha,wizi wa mali na fedha taslimu na walitumia silaha za moto ikiwa ni pamoja na bunduki aniana ya SMG, bastola na vifaa mbalimbali vya uvunjaji ikiwa ni pamoja na baruti.
Aliongeza kuwa watuhumiwa waliokamatwa kwa tukio la kuuwawa kwa mtawa ni Manase Ogenyeka (35) mkazi wa Tabata Chang’ombe ambaye ni muendesha bodaboda na Hamisi Shabani Mfanyabishara ,mkazi wa Magomeni Mwembechai.
Alisema tukio la kuuwawa kwa mtawa wa kanisa katoliki Crisencia Kapuri (50) ambaye pia alikuwa muhasibu wa parokia ya Makoka kilitokea Juni 23 eneo la ubungo Kibangu.
Aidha majambazi hawa wawili licha ya kuhusishwa  na tukio la kifo cha mtawa na kupora Sh milioni 20 piwa walikuwa wakitafutwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za uporaji wa Benki ya Barclays tawi la Kinondoni  lililotokea Aprili 28 ambapo mamilioni ya fedha yaliibiwa kabla na baada ya tukio.
“Jambazi Manase Ogenyeka ndio alieendesha pikipiki akimbeba jambazi mwenzake akiwa na fuko la mamilioni ya fedha na kutoroka nazo wakati jambazi Hamisi Shabani  ndiye aliyekuwa kiongozi katika tukio hilo” alisema Kova.
Alisema jeshi la polisi bado linawatafuta wathumiwa wengine wawili katika tukio la Mtawa na jambazi mmoja jina maarufu Leonard Molel katika tukio la benki ya Barclays.
Majambazi wengine watatu kati ya hao nane waliokamatwa walikamatwa baada ya kutumia mbinu ya hati bandia wakiwa wanaoomba kazi katika kampuni binafsi ya ulinzi iitwayo INSTANT SECURITY SERVICES iliyopo mtaa wa Makangira Msasani.
Ambao ni Elibariki Makumba (30) mkazi wa Buguruni Madenge, Nurdin Suleimani (40) mkazi wa Buguruni Madenge,na Mrumi Salehe(38) mkazi wa Kigogo fresh.
“Majambazi hawa walikuwa wanaomba kazi ya ulinzi ili badaye waweze kutenda uhalifu wao wenyewe au wawaruhusu wanamtandao wenzao waweze kutenda uhalifu kwa urahisi”aliongeza Kova.
Pia alitoa rai kwa Makampuni ya ulinzi kwamba wanapotaka kuajiri washirikiane moja kwa moja na jeshi la polisi ili wafanye upekuzi wa pamoja utakaohusisha alama za vidole,picha na ukaguzi wa kumbukumbu muhimu za kibayologia kama vile vipimo vya DNA.
Aliongeza kuwa wanawaomba wananchi ambao wanatabia ya kutembea na fedha nyingi waache kwani kwa sasa tekinolojia imekuwa wanaweza kutumia simu na kuhamisha fedha kwenda benki moja kwenda nyingine.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles