Mshambuliaji wa Uholanzi, Arjen Robben akiwa ameangushwa chini na hivyo kuipatia timu yake penalti dhidi ya Mexico katika mechi ya Kombe la Dunia hatua ya 16 Bora jana. Penalti hiyo ilipigwa kiufundi na Klaas-Jan Huntelaar na kuivusha Uholanzi hatua ya Robo Fainali ambapo itapambana na Costa Rica iliyoitoa Ugiriki kwa penalti 5-3.