Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4605

COSTECH YAFADHILI MAKUNDI BUNIFU 26 YA UZALISHAJI

$
0
0
Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) imetoa zaidi ya Sh milioni 200 kusaidia kongano bunifu  26 zinazozalisha na kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali  hapa nchini kwa kipindi cha miaka minne iliyopita.
Msaada huo unalenga kuchochea ubunifu na ushindani wa soko kwa kuwezesha kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali zikiwa na ubora na viwango vya kimataifa.
Hayo yalisemwa na Mtafiti ambaye pia ni Mratibu wa Mafunzo kutoka  Tume hiyo Furaha Kabuje juzi mjini hapa kabla ya Mkuu wa Mkoa huo, Joel Bendera, kufunga mafunzo ya kongano bunifu wa bidhaa za aina mbalimbali nchini.
Kabuje alisema tume hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sayansi na teknolojia inawasaidia wananchi,  na kwamba  kongano zitakazoonyesha juhudi binafsi ndizo zinazosaidiwa kwa kupatiwa Sh milioni nane kila moja ili ziwasaidie kutekeleza mipango ya kuendeleza kongano zao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa Bendera, aliwataka washiriki hao kutumia ujuzi na maarifa waliyoyapata katika kuendeleza kongano mbalimbali nchini, ili waingie katika ushindani wa biashara utakaokidhi viwango vya  soko la kimataifa.
Alifafanua kwamba Serikali itaendelea kuunga  mkono na kushiriki
kikamilifu katika juhudi za kuendeleza kongano kwa kuwa zimeonyesha mafanikio makubwa  katika kuongeza pato la taifa , ajira na maendeleo ya jamii.
Naye mwakilishi wa kongano la mafuta ya alizeti kutoka mji mdogo wa Kibaigwa, wilayani Kongwa, mkoani Dodoma, Ringo Iringo, aliipongeza Tume hiyo kwa kufadhili mafunzo hayo ambayo ni chachu ya mabadiliko ya kibiashara yatakayolenga uzalishaji ubora wa bidhaa.
Mafunzo hayo ya siku nne, yaliwashirikisha wawakilishi wa kongano za ubunifu wa bidhaa mbalimbali kutoka mikoa ya Arusha, Kigoma, Dodoma, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Kilimanjaro na Morogoro.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4605

Trending Articles