Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro,imetoa hundi yenye thamani ya Sh milioni 22 kwa vikundi vya Wajasiriamali vya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) viendeleze shughuli za uzalishaji mali utakaowapatia vipato na maisha bora.
Mratibu wa Ukimwi katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Florence Mwambene, alisema kutolewa kwa fedha hizo ni kuviwezesha vikundi hivyo kujitegemea kiuchumi.
Hata hivyo alivitaja vikundi vilivyokabidhiwa fedha ni pamoja na Mtandao wa Watu wanaishi na VVU wilaya ya Morogoro uliopatiwa hundi ya Sh milioni 20, Tushikamane Vijana Sh milioni moja sambamba na Tushikamane Wanawake waliopatiwa kiasi kama hicho.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Ukimwi wa Halmashauri hiyo, kwa
kushirikiana na jamii pamoja na Asasi zingine ilianza uundaji wa vikundi vya watu wanaoishi na VVU tangu mwaka 2008/2009.
"Tulianza na vikundi vitatu ambavyo ni Waviumka Kata ya Mkambarani, Waviunge Kata ya Ngerengere na Upenzo Moro V Kikundi cha watumishi," alisema Mratibu huyo.
Hata hivyo alisema, katika Halmashauri hiyo kuna vikundi 160 kati ya hivyo 100 vya wanawake na 60 vya vijana vinajishughulisha na kazi mbalimbali za uzalishaji mali.
Mratibu huyo Ukimwi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, alizitaja shughuli hizo ni pamoja na ufugaji, kilimo na kufanya biashara kwenye masoko na kwamba miradi hiyo itawawezesha kukabiliana na kuondokana na utegemezi na kubadilishana uzoefu wao kwa wao.