Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

WAKATI MATOKEO RASMI KUTANGAZWA KESHO, UHURU KENYATTA AZIDI KUTIMUA VUMBI...

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya, Ahmed Isaack Hassan.
Matokeo yaliyotufikia ya kura za kiti cha Urais Kenya yanaonesha kwamba Uhuru Kenyatta bado anaendelea kumtimua vumbi kuelekea Ikulu kwa kuzoa jumla ya kura 2,761,877 ambazo ni asilimia 52.41 ya zilizohesabibiwa mpinzani wake wa karibu Raila Odinga akijikusanyia kura 2,173,347  ambazo ni asilimia 42.02 hadi kufikia mida ya Saa 03:00 usiku huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo, Ahmed Isaack Hassan, mbele ya vyombo mbalimbali vya habari, matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa mapema kesho na kwamba maofisa watafanya kazi ya kuhesabu na kuhakiki matokeo hayo usiku mzima wa leo.
Endelea kuperuzi ziro99blog. Pia tazama matangazo ya televisheni ya KTN moja kwa moja ndani ya blogu hii inayokuja kwa kasi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

Trending Articles