Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

SEKRETARIETI YA AJIRA YABAINI VYETI 1,035 VYA KUGHUSHI

$
0
0
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeshabaini  vyeti vya kughushi  1,035 kutoka kwa baadhi ya waombaji  kazi tangu  mpango wa kuhakiki vyeti ulipoanza hadi  mwezi  Mei mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Sekretarieti ya Ajira, Riziki Abraham  kwenye Maonesho ya Utumishi wa Umma, yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Riziki alisema katika vyeti hivyo vya kughushi vilivyobainika, 661 ni vyeti vya shule za sekondari, ambavyo wahusika wanadai kuvipata kutoka Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), leseni  tatu za udereva, vyeti 257  vya udereva, ambavyo wahusika wanadai kuvipata kutoka vyuo vya Mafunzo ya Ufundi (VETA) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT), vyeti 86 vya kuzaliwa na vyeti 28 vya taasisi mbalimbali.
Pia, alisema katika mwaka wa fedha wa 2013/14, Sekretarieti ya Ajira, ilifanikiwa kujaza  nafasi sita za maofisa watendaji wakuu, nafasi 65 za wakurugenzi na wakuu wa idara na nafasi 27 za wakuu wa vitengo wa Wakala wa Serikali na taasisi za umma.
Riziki alisema Sekretarieti  ya Ajira katika Utumishi wa Umma, inatumia njia mbalimbali katika kuwasiliana na wadau wake, ikiwemo kutoa taarifa za uendeshaji wa mchakato wa ajira serikalini. 
“Matangazo  ya kazi na taarifa mbalimbali hutolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kama vile tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni   www.ajira.go.tz, ukurasa wa face book  wa ‘Sekretarieti  ajira’, runinga, redio, magazeti, majarida, vipeperushi  na ushiriki katika semina  na kongamano  mbalimbali,” alisema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles