Mume wa Mwimbaji wa nyimbo za injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili ya ubakaji.
Mshitakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji, alipanda kizimbani jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai Mei 23 mwaka huu, maeneo ya Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala mshitakiwa alitenda makosa mawili
Katika shitaka la kwanza, anadaiwa maeneo ya Tabata Kimanga wilayani Ilala, alimbaka shemeji yake.
Katuga alidai Mei 25 mwaka huu, maeneo ya Tabata Kimanga, alimbaka tena mfanyakazi wake wa ndani.
Mshitakiwa alikana mashitaka na alirudishwa rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.
Alitakiwa kuwa na wadhamini wawili, kutoka taasisi za Serikali watakaosaini kulipa sh milioni tano. Kesi itatajwa Juni 19 mwaka huu.