Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

SERIKALI YATAMBA KUWANASA WALIPUAJI MABOMU ZANZIBAR

$
0
0


Serikali imesema ina uwezo wa kuwakamata wale wote waliohusika katika shambulizi la bomu lililosababisha kifo na kujeruhi wengine saba mwishoni mwa wiki iliyopita, mjini Zanzibar.
Wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, akitoa msimamo huo, polisi imesema kutokana na uchunguzi unavyoendelea, polisi itabaini mengi zaidi. 
Hayo yalielezwa jana visiwani hapa, Naibu  Waziri alipotembelea mmoja wa majeruhi anayeendelea na matibabu kwenye Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, mjini Zanzibar.
Naibu Waziri alisema, alisema polisi wanao  uwezo mkubwa wa kupeleleza na kukamata; isipokuwa  kinachohitajika ni kupatiwa taarifa sahihi na kwa wakati wazifanyie kazi. 
Alisema serikali imekuwa ikisikitishwa na matukio hayo ya milipuko ya mabomu pamoja na mengine ya kihalifu kutokana na kuzorotesha hali ya usalama wa taifa letu.
Alisema miongoni mwa wananchi, lazima yupo  mtu ama watu wanaowafahamu wahusika na kwamba wakitoa ushrikiano kwa Polisi, waliohusika watatiwa nguvuni  na kukabiliwa na mkono wa sheria.
"Uwezo wa kupeleleza na kuwapata wote waliohusika tunao, tunachohitaji kama serikali,  ni kupata taarifa sahihi za wahusika ili tuzifanyie kazi kwa makini," alisema. 
Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (DIGP) Abrahamani Kaniki, alisema ingawa uchunguzi unaendelea, polisi imebaini bomu lililotumika katika shambulio hilo, limetengenezwa kiwandani tofauti na taarifa za awali kuwa lilitengenezwa kienyeji.
Kaniki alisema kutokana na uchunguzi unavyoendelea, polisi itabaini mengi zaidi. “Lakini kwa sasa itoshe kusema kuwa Jeshi la Polisi limebaini kuwa bomu la kivita,” alisema.
Kiongozi huyo wa polisi ametaka Watanzania kuendelea kuamini Jeshi la Polisi. Alisema limejipanga kikamilifu kuhakikisha wote waliohusika kwa njia moja au nyingine, wanakamatwa.
Alisema mbali ya mapambano hayo, polisi inaangalia njia itakayoweza kusaidia kuzua matukio makubwa kabla ya kutokea. 
"Kama mnavyojua kukinga ni bora zaidi kuliko kutibu," alisema DIGP Kaniki na kuongeza kuwa ingawa inaweza kuchukua muda kidogo, anayo imani waliotenda uhalifu huo watapatikana. 
Aidha alisema polisi inaendelea kufanya uchunguzi wa kina kubaini bomu hilo lilitoka wapi na liliingiaje nchini. Hata hivyo alisema mipaka ya nchi ni mipana. 
"Itoshe kusema kuwa tunafanya uchunguzi na tutaujulisha umma pale ambapo itabidi bila ya kuathiri hali ya usalama wa nchi," alisisitiza DIGP Kaniki kabla ya kutembelea majumbani baadhi ya majeruhi walioruhusiwa kutoka hospitalini. 
Ziara hiyo ililenga kujulia hali majeruhi na kusikia ushuhudia wa kilichowapata siku ya tukio. 
Matamko hayo ya Naibu Waziri na DIGP yamekuja siku chache tangu Rais Jakaya Kikwete alipotaka jeshi la polisi kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki watu wote waliohusika katika ulipuaji bomu lililosababisha kifo na kujeruhi watu saba mjini Unguja, Zanzibar. 
Kikwete ambaye alisema  kitendo hicho ni cha kulaaniwa kwa nguvu zote na watu wote wapenda amani Bara na Visiwani,  alisema kitendo hicho si cha kistaarabu, kisichokubalika katika dunia ya sasa. 
Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai wa Zanzibar, Yussfu Ilembo, aliyekufa papo hapo ni Muhammad Mkombalaguha (26), mkazi wa Tanga.
Mtu huyo aliyekufa papo hapo pamoja na majeruhi, walikutwa na mkasa huo  wakitoka Msikiti wa Darajani baada ya Ibada ya Swala ya Isha inayoswaliwa kuanzia saa 1:45 usiku na kuendelea. 
Baada ya kumalizika ibada hiyo, walitoka msikitini na kufika eneo la Darajani wakisubiri gari na ndipo mlipuko mkubwa uliposikika ambao unasadikiwa kuwa ni bomu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles