Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka juzi alinusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Bukoba kwenda Dodoma kupata ajali kwa kugonga punda katika Kijiji cha Wendele wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo ilitokea juzi saa 11.07 jioni likijumuisha gari namba STK 5857 alilokuwa akisafiria Waziri huyo akiwa na familia yake likiendeshwa na Linusi Eliasi (42).
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Kihenya Kihenye alisema baada ya kufika katika eneo hilo, alikatisha punda katikati ya barabara na katika harakati za dereva kumkwepa mnyama huyo, gari hilo lilimgonga akafa papo hapo.
Alisema hakuna mtu aliyeumia isipokuwa, baadhi ya abiria wa gari hilo, walipata majeraha madogo madogo. Aidha Waziri Tibaijuka alipata mshituko lakini baadaye hali yake iliendelea vizuri.
Hata hivyo msafara wa Waziri na wengine aliokuwa nao, walilala mjini Kahama na jana asubuhi, uongozi wa Serikali wa Wilaya, ulimpatia usafiri mwingine kumpeleka mjini Dodoma anakohudhuria vikao vya Bunge.