Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umesitisha safari za treni ya abiria kutokana na kutetereka kwa mojawapo ya madaraja katika Bonde la Mto Ruvu katika reli ya kati.
Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kipallo Kisamfu, safari zimesitishwa kuanzia juzi.
“Tunawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na kutetereka kwa mojawapo ya madaraja katika Bonde la Mto Ruvu katika reli ya kati, tumeamua kusitisha kwa muda huduma ya usafiri wa abiria hadi ukarabati wa daraja utakapokamilika,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, juzi Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kisamfu na Wahandisi Waandamizi na Mafundi Mchundo Ujenzi walifika katika daraja hilo na kulifanyia tathmini kuona uharibifu uliotokea na mahitaji kuliimarisha ili lirejee katika kiwango cha usalama kuruhusu treni za abiria kupita.
Imeeleza ukarabati wa kulirejesha katika hali ya kutumika itachukua takribani wiki moja kuanzia juzi saa 12 jioni huduma ilipositishwa kati ya Dar es Salaam na daraja hilo.
Kwa taarifa hiyo, abiria ambao walikuwa wasafiri kwenda bara kwa treni ya juzi, waliarifiwa kufika katika stesheni zilizo karibu warejeshewe nauli zao watafute usafiri mbadala.
Taarifa hiyo ya kampuni ilisema tangu juzi, kazi ya kurejesha nauli kwa abiria wapatao 1,000 iliendelea katika stesheni mbalimbali za TRL na hasa katika Stesheni kubwa ya Dar es Salaam ambapo safari kwenda bara huanzia. Uongozi wa TRL umeomba radhi kwa abiria kwa usumbufu uliojitokeza.