Jamaa mmoja eneo la Posta Mpya ghafla katupa chini simu yake na kuanza kutimua mbio baada ya kuona gari la moja ya kampuni za simu za mikononi likikatiza mbele yake. Wakati abiria kituoni hapo wakiwa na mshangao, jamaa huyo akarejea baada ya dakika chache huku akitweta na kusema: "Mungu mkubwa! Unajua nimekopa salio katika simu yangu kwenye mtandao wa wale jamaa (huku akionyooshea kidole lilipoelekea lile gari) tangu juzi bado sijalipa." Kasheshe...
↧