Biashara ya ngono kuingiliana kinyume na maumbile pamoja na matumizi ya dawa za kulevya vimetajwa kuwa kikwazo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi.
Mwakilishi wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids), Dk Paul Maiga alisema hayo kwenye warsha ya siku mbili kwa wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Tabora, Shinyanga, Simiyu na Singida juu ya Mkakati wa tatu wa taifa wa kudhibiti ugonjwa huo.
Dk Maiga alisema licha ya kasi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo kupungua kutoka asilimia saba mwaka 2003 hadi asilimia 5.1 mwaka juzi, takwimu za kitaifa zinaonesha makundi yalioainishwa, maambukizi yamepanda hadi zaidi ya asilimia 40.
Kutokana na hali hiyo, mwakilishi huyo kutoka Tacaids alisema pamoja na mambo mengine yaliyoainishwa katika mkakati huo, ni vema kila halmashauri nchini ikaelekeza nguvu zaidi katika kupunguza maambukizi kwa makundi hayo maalumu.
Hata hivyo, mapendekezo ya wadau katika kukabiliana changamoto hiyo ni kurekebisha sheria zilizopo ili kudhibti biashara ya ngono.
Kwa mujibu wa Dk Maiga, usambazaji wa Mkakati wa Tatu wa Taifa kwa ajili ya kudhibiti Ukimwi nchini, unalenga kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hadi kufikia asilimia 0.16 ifikapo mwaka 2018.