Bondia kutoka Iran, Gavad Zohrev ametuma salamu kwa Francis Cheka kuwa hazungumzii mengi, kwani amejipanga kuchukua ubingwa katika pambano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa PTA katika Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam.
Zohrev alisema jana Dar es Salaam tayari ameshajua mbinu za mpinzani wake Cheka katika CD hivyo anajua ni jinsi gani atamkabili.
“Nimeshamwona, najua kwamba ni mrefu kuliko mimi, ninajua nitatumia mbinu kumkabili, nimejipanga mambo yatakuwa sawa,” alisema bondia huyo wa Iran.
Alisema kutokana na ufupi wake, atapigana kwa kutumia mtindo wa bondia wa zamani wa Marekani, Mike Tyson.
Alisema pambano hilo sio la kwanza kushiriki, ameshacheza mapambano 14 katika nchi mbalimbali za Ulaya na Asia na kupoteza mchezo mmoja. Kati ya hayo, moja lilifanyika Urusi ambako alipata medali ya shaba.
Naye Promota Jay Msangi alisema Cheka atakuwa na kibarua kizito siku hiyo, kwani bondia huyo anajiamini na kujipanga kuchukua ubingwa.
Alisema mabondia wote wataanza kupima uzito leo kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) na kuzungumza na waandishi wa habari.
Msangi alisema maandalizi yote yamekamilika, bondia atakayepambana na Francis Miyusho, Angelito Merin, atakuwepo leo kwani alitarajiwa kutua jana mchana.