Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4561

SITTA AVUNJA KAMATI YA UONGOZI BUNGENI...

$
0
0
Samuel Sitta akiongoza Bunge la Katiba.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta ametengua uteuzi wake wa awali wa nafasi tano za Kamati ya Uongozi ili kuifanya kamati hiyo kuwa na uwakilishi mpana.

Akitangaza hatua hiyo bungeni jana, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan alisema Sitta ametumia Kanuni namba 58 fasihi ya Kwanza C, inayotaka matakwa ya kanuni kuzingatia uwakilishi mpana wa Bunge hilo.
Alisema kupitia kanuni ya 58 (D), Mwenyekiti huyo wa Bunge Maalumu la Katiba anakiri kuwa uteuzi wa awali haukuzingatia vema uwakilishi uliopo ndani ya Bunge hilo na kwamba baada ya majadiliano na wadau ameamua kutengua uteuzi huo.
Sitta alitangaza uteuzi wa awali Machi 25, mwaka huu, alipowateua wajumbe watano ili waweze kuungana na wenyeviti 14 wa kamati za Bunge ili kukamilisha idadi ya wajumbe 19 wanaounda Kamati ya Uongozi ambayo ndiyo inayoratibu shughuli zote za Bunge hilo.
Katika uteuzi uliotenguliwa, Sitta aliwatangaza Fakharia Shomari, Mary Chatanda, Hamoud Abuu Jumaa, Amon Mpanju na Profesa Ibrahim Lipumba kuingia kwenye Kamati ya Uongozi kupitia nafasi tano za uteuzi wa Mwenyekiti. Hata hivyo, Profesa Lipumba alikataa uteuzi wake.
Katika uteuzi mpya wajumbe waliopata nafasi ya kuingia kwenye Kamati hiyo ni Freeman Mbowe,  Fatuma Abdulhabib Fereji, Nakazael Tenga, Amon Mpanju na Aboubakar Khamis Bakary.
Mara baada ya uteuzi wake wa awali wa Machi 25, mwaka huu, wajumbe mbalimbali walipinga uteuzi wa Mwenyekiti Sitta, wakidai kuwa haukuzingatia usawa wa makundi yanayounda Bunge hilo na kuifanya Kamati hiyo kujaa wajumbe wengi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hatua hiyo pamoja na mambo mengine, ililalamikiwa na wajumbe wengi waliochangia kwamba ingeifanya CCM kuhodhi mwenendo mzima wa uendeshaji wa Kamati hiyo,  huku Mjumbe Kangi Lugola akimuomba Mwenyekiti Sitta kutengua uteuzi huo, kutokana na wanaCCM kuwa wengi ili kuleta usawa na kuondoa uwezekano wa hisia za haki kutofuatwa.
Miongoni mwa waliopinga pia uteuzi wa awali ni Mjumbe John Mnyika, ambaye pamoja na kusimama na kupinga bungeni alikata rufaa kwa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge hilo, kupinga hatua hiyo ya Sitta, rufani ambayo ilitolewa uamuzi jana.
Akisoma majibu ya rufani hiyo jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge, Pandu Ameir Kificho alisema baadhi ya hoja za rufani ya Mnyika, zilizingatiwa na baadhi hazikuzingatiwa na ndio kiini cha kufanyika kwa mabadiliko ya Kamati hiyo ya Uongozi jana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4561

Trending Articles