Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630

MKAZI WA MOSHI ABAMBWA AKIFANYA MAPENZI NA MBWA...

$
0
0
Mbwa.
Katika hali ambayo ni ya kushangaza, mkazi wa Kata ya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, anadaiwa kukutwa akifanya ngono na mbwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alitaja jina la mtu huyo (jina tunalihifadhi), akisema  anadaiwa kukutwa akifanya kitendo hicho usiku wa kuamkia  jana kwenye chumba chake.
Kamanda Boaz alisema majirani zake, ndiyo walishuhudia na kutoa taarifa polisi. Mtuhumiwa anadaiwa kukimbia kusikojulikana.
Mbwa huyo anamilikiwa na mtoto wa mtuhumiwa.
Kwa mujibu wa kamanda, mtuhumiwa ana familia ya wake watatu. Polisi inamtafuta mbwa husika  kumfanyia uchunguzi.
Akizungumza na mwandishi jana, Daktari wa Hosptali ya Rufaa ya KCMC,  alisema mtu anayefanya kitendo hicho na mnyama, anahitajika kufanyiwa vipimo, kubaini kama yuko sawa.
"Kwa kawaida sio jambo la kawaida, anaweza kuathirika kisaikolojia na jamii kumchukulia mtu wa tofauti kama amelaaniwa au ni kichaa, pengine
anahitajika kufanyiwa vipimo kuonekana kama yupo sawa," alisema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630