Wabunge wa Bunge la Uganda juzi wamezua tafrani baada ya kuibua hoja ya kutaka waongezewe mishahara, ambapo tayari mshahara yao ni mara 60 ya mshahara wa mfanyakazi wa umma.
Ombi hilo limekuja wakati ripoti ya mkaguzi mkuu ikiwalalamikia viongozi waandamizi wa serikali na Wabunge kushindwa kuthibitisha matumizi ya mamilioni ya dola.
"Tumepokea maombi kutoka tume ya bunge wakitaka nyongeza ya mwaka ya sh milioni 11 za Uganda (dola za marekani 4,486), lakini tunasubiri majibu kutoka wizara ya fedha," afisa wa Bunge la Uganda, Jane Kibirige aliiambia AFP.
Ombi hilo limeibua hasira za wananchi kupitia mitandano ya kijamii, wakilalamikiwa wawakilishia wao kujilimbikizia fedha wakati mtumishi wa serikali wakipewa dola za marekani 100 kwa mwezi na kiwango kidogo zaidi kwa watumishi wa umma.
"Kwa sasa tunalipwa shilingi ya Uganda milioni 15 (dola 6,100) kwa mwezi. Inawezekana vipi kuja na pendekezo la nyongeza?” alilalamika Mbunge na kiongozi mwandamizi wa upinzani Ken Lukyamuzi.
"Hii ni kama kunyonya uchumi na kuwanyanganya wananchi huduma wanazohitaji. Suala hili halifai kabisa.”
Mbali na mishahara, Wabunge wa Uganda pia upewa posho mbalimbali ikiwa ni pamoja na gharama za usafiri na fedha za kununulia gari binafsi.
Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Daily Monitor, Mkaguzi mkuu wa Uganda amepigia kelele juu ya matumizi ya dola za marekani milioni 25 zilizotumiwa na viongozi waandamizi, ikijumuisha dola za marekani milioni 15 kama gharama za usafiri kwa wabunge ambazo zimeshindwa kuthibitishwa matumizi yake.
Uganda imekuwa ikilalamikiwa mara kwa mara juu ya kukithiri kwa rushwa, na nchi pia inakabiliwa na tishio la kufutiwa misaada ya kigeni baada ya kupitisha sheria ya kupambana na vitendo vya ushoga na usagaji.