Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4561

SUPERMARKET 39 ZAFUNGIWA KWA KUUZA BIDHAA HATARISHI...

$
0
0
Relentless, moja ya bidhaa zilizopigwa marufuku.
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imefungia maduka makubwa 39, yakidaiwa kuuza vyakula hatarishi kwa afya na uhai wa binadamu.

Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, amesema miongoni mwa bidhaa zilizokutwa katika maduka hayo kupitia operesheni iliyoendeshwa kati ya Machi 10 na 20 mwaka huu, ni maziwa ya kopo, chumvi na vinywaji vya kuongeza nguvu. 
Bidhaa  katika maduka hayo,  baadhi yake zilibainika kuwa bandia, zisizo na ubora. Nyingine zilikutwa zikiwa na vifungashio vilivyoandikwa lugha  ya kigeni, isiyoeleweka kwa walaji wengi. 
Alitaja majina ya baadhi ya  maduka husika yaliyoko jijini Dar es Salaam,  na kusema sheria itachukua mkondo wake kuhakikisha inakuwa mfano.
Kwa upande wa maziwa ya kopo, taarifa ya mkurugenzi huyo kwa waandishi wa habari, inasema yamekamatwa 591 yenye thamani ya Sh milioni 17 na utaratibu wa kuyaharibu unaandaliwa.
Alitaja majina ya maziwa hayo ni  SMA 1, 2 and 3, Promol Gold, S-26 Gold, Nursoy, Progress Gold, Cow & Gate, Isomil 2, InfacareSoya, Nutrikids na Aptimil 1.
“Maziwa hayo pamoja na kuwa hayajasajiliwa, lakini pia yalifungwa kwenye vifungashio vyenye lugha isiyoeleweka na  ingawa uchunguzi unaonesha lugha hiyo ni kichina. Hiyo ni kinyume cha sheria ya vifungashio vya vyakula inayohimiza vyakula vyote kuambatana na maelekezo kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza zinazoeleweka kwa walaji wengi,” alisema.
Alitaja bidhaa nyingine zilizokamatwa kwenye kwenye operesheni iliyoendeshwa kati ya Machi 10 na 20  mwaka huu, jijini Dar es Salaam, ni vinywaji vya kuongeza nguvu mwilini makopo 1,526.
Vinywaji hivyo ni aina ya Monster, B52, Krazy, Relentless, Boost, Red bull toleo la red, Silver na Blue, Rockstar, Climax na Atlas vyenye thamani ya Sh milioni 4.5.
Aidha TFDA imekamata paketi 6,090 za chumvi zenye thamani ya Sh milioni tano; ikidaiwa kuwa bandia.
Alitaja majina yaliyo kwenye paketi hizo ni Lo Salt, American Garden Salt, Kensalt, Saxa, Chilly Willy Salt, Today’s Essential, Best Salt Nezo Salt, DP na  Costa Salt ambazo pia zinasubiri kuharibiwa kwa mujibu wa sheria.
Kwa mujibu wa Sillo, pamoja na juhudi za kutoa elimu juu ya utaratibu bora wa biashara za vyakula kwa wafanyabiashara na wamiliki wa maduka ya vyakula, adhabu kali zitatolewa kwa wote walionaswa kwenye operesheni.
Alisema wanataka kutoa fundisho kwa wengine hii, ikiwa ni pamoja na kuharibu vyakula kwa gharama zao wenyewe.
Imeelezwa tatizo la uholela wa biashara ya maduka makubwa hususani jijini Dar es Salaam, ni kubwa. Meneja wa TFDA Kanda ya Mashariki, Emanuel Alphonce, alisema Mamlaka inajiandaa kuja na mkakati wa kudumu juu ya suala hilo.
“Kuna tatizo. Unaweza kukuta leo maduka kama kumi yamefungwa, lakini ukipita wiki nyingine unakuta mengine idadi kama hiyo yanafanya kazi lakini Mamlaka haina taarifa nayo. Tunalifanyia kazi tatizo hilo kwa kuimarisha uchunguzi na udhibiti,” alisema Alphonce.
Alihimiza wateja wa bidhaa za vyakula, kuongeza umakini wakati wa kununua vyakula hasa kwenye maduka hayo ambayo yanashabikiwa na wengi mjini.
Alitaka wajenge utamaduni wa kuchunguza tarehe ya mwisho wa matumizi pamoja ma maelekezo kwenye vifungashio.
Kwa mujibu wa Sillo, wananchi wanatakiwa kuwa makini pia na chumvi inayofaa kwa matumizi na kuongeza chumvi inayofaa ni ile iliyoandikwa maneno ya Iodated Salt na siyo yenye maneno Iodazed Salt.
Alikumbusha jamii kujenga  utaratibu wa kutunza risiti za bidhaa  ikitokea matatizo iwe rahisi kupeleleza na kuchukua hatua.
“Wafanyabiashara wanaouza maziwa ya watoto, vinywaji vya kuongeza nguvu  na bidhaa nyingine mpya zinazosambazwa katika makuka yao, wanatakiwa kununua bidhaa zilizosajiliwa vinginevyo watachukuliwa kuwa ndio walioingiza bidhaa hizo,” alionya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4561