Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

TCU KUKAGUA UBORA WA HUDUMA VYUO VIKUU...

$
0
0
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) itakagua huduma zitolewazo kwenye vyuo vikuu, kabla ya taasisi hizo kuamua kupitisha ada.
Kaimu Katibu Mkuu wa TCU, Profesa Magishi Mgasa alisema hatua hiyo inalenga kuhakikisha gharama ambazo mwanafunzi analipia, ndizo zinazotolewa.
“Hakuna chuo kitakachotangaza ada ya kozi mpaka ithibitishwe na TCU, hapo tutaangalia huduma zinazotumika kukokotoa ada ndizo zinazotolewa. Haiwezekani tukakuta chuo kinasema kina maabara 10 wakati wanayo moja, tutahakiki na kujiridhisha,” alisema Mgasa.
Mwezi uliopita, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alizindua mfumo wa gharama halisi kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambao umepangwa kuanza mwaka ujao wa masomo wa 2014/2015.
Mgasa alisema mfumo wa gharama halisi ya masomo kwa mwanafunzi wa elimu ya juu,  unajumuisha gharama zote za kuendesha kozi husika kwa mwaka, zitakazokokotolewa kwa kuzingatia mishahara ya wafanyakazi wote wa chuo husika na huduma nyingine.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles