![]() |
Spika wa Bunge la Afrika Kashariki akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete na Spika Anne Makinda. |
Bunge la Afrika Mashariki (EALA), limeahirishwa kwa muda usiojulikana baada ya kutawaliwa malumbano jana juu ya suala zima la kumng’oa Spika.
Malumbano ya kisheria ya kutaka kumng'oa Spika, Dk Margareth Zziwa, yalijitokeza jana baada ya kuwapo pande mbili, zilizopingana juu ya suala hilo.
Baadhi ya wabunge walidai hoja hiyo, haiwezi kujadiliwa kwa vile ipo mahakamani. Wengine walisema inaweza kujadiliwa bila tatizo lolote.
Kutokana na malumbano hayo, Zziwa aliahirisha Bunge hilo kwa muda usiojulikana.
Hali tete bungeni ilianza kujitokeza mapema jana mchana, kabla ya kuanza kwa kikao hicho. Wakati kawaida kikao huanza saa 8: 00 mchana, jana kilianza saa 9:45 alasiri na kumalizika saa 10:03 jioni.
Hali hiyo ilitokana na wabunge wengi kuwa nje ya ukumbi, badala ya kuingia ukumbini. Waligongewa kengele, lakini hawakuingia.
Hata ilipopigwa kengele nyingine, kutaka waingie, meza zao zilikuwa zimewekwa karatasi za shughuli za kazi kwa siku hiyo, huku hoja ya kumng'oa Spika bila kuwemo.
Ilielezwa karatasi hiyo, iliondolewa muda mfupi kabla ya kuanza kwa Bunge ;na waligawiwa karatasi nyingine, zilizoonesha kuwa na hoja ya kumng'oa Spika.
Baada ya sala iliyosomwa na Spika, Katibu wa Bunge hilo, Kenneth Madete, alimtaka mtoa hoja, Peter Mathuki, kusoma hoja yake.
Lakini, wakati akifanya hivyo, Mbunge kutoka Uganda, Fred Mbidde, aliomba utaratibu kwa Spika.
Aliporuhusiwa, Mbidde alipinga kuwasilishwa kwa hoja hiyo kwa maelezo kwamba lipo shauri, lililowasilishwa Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ), kutaka ufafanuzi kuhusu utaratibu wa kumng'oa Spika ulivyo.
Mbidde alisema wakati wakisubiria uamuzi wa Mahakama, si vyema kwa Bunge hilo kujadili tena hoja hiyo.
Hoja hiyo ilipingwa na Mwanasheria wa Afrika Mashariki, Wilbard Kahwa, aliyesema pamoja na shauri hilo kuwa mahakamani, haimaanishi wabunge kutojadili.
Malumbano kati yao yaliendelea huku wabunge wa pande mbili, wakipigia makofi hoja wanazounga mkono. Ndipo Spika Zziwa, aliamua kuahirisha Bunge hilo kwa muda usiojulikana.
Nje ya ukumbi wa Bunge, baadhi ya wabunge walisema hawana imani na uongozi wa Zziwa, kutokana na kuwa na upendeleo wakati wa kupanga safari za nje.
Ilidaiwa miongoni mwa wabunge, baadhi wanajirudia katika ziara huku wengine wakipata safari chache.
Mkakati wa kumng’oa spika huyo, ulianza hivi karibuni kwa wabunge wanne kutoka kila nchi mwanachama, kusaini hati ya kusudio hilo na kuwasilisha kwa Katibu wa Bunge, Madete.
Uamuzi wa kumng’oa Spika huyo wa Bunge, lenye wabunge 45, unatokana na madai kwamba ameshindwa kufanya kazi kwa viwango, ikiwemo upendeleo miongoni mwa wabunge.