Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

WAJUMBE WAPIGWA BUTWAA KUVUNJWA BUNGE MAALUMU LA KATIBA...

$
0
0
Lango Kuu la kuingilia katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Ukimya mkubwa umetanda kwenye viwanja vya Bunge kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kushindwa kuamini wanachokisoma kwenye tangazo lililobandikwa katika lango kuu la kuingilia ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Tangazo hilo ambalo liliwaacha baadhi ya wajumbe wakichuruzika machozi bila kujijua lilikuwa likiwataka wajumbe hao kufungasha virago vyao ndani ya masaa matatu na kurejea makwao.
Hatua kwa mujibu wa tangazo hilo, imekuja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kutangaza kulivunja rasmi bunge hilo kufuatia kutawaliwa na malumbano yasiyokuwa na tija kwa taifa.
Katika tangazo hilo, wajumbe hao pia wametakiwa kurejesha ndani ya mwezi mmoja posho zote walizokwisha kulipwa hadi sasa kwakuwa fedha hizo ni mali ya wananchi.
Mpaka sasa, inakadiriwa kwamba kila mjumbe ameshalipwa takribani Shilingi milioni 12, na kwamba fedha hizo zinatakiwa kuwa zimeshalipwa hadi kufikia mwisho wa mwezi Aprili.
Hakuna mjumbe yeyote aliyekuwa tayari kuzungumza na blogu hii kutokana na kila mmoja kuonekana 'bize' akijadiliana na mwenzake huku wajumbe wa kike wakionekana wamejiinamia kwa uchungu baadhi wakilia kwa kwikwi.

Hakika ni Aprili Mosi ambayo haitakaa ikasahaulika vichwani mwa Watanzania wengi!

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles