Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

WACHINA WA 'SAMAKI WA MAGUFULI' WAPANDISHWA TENA KORTINI...

$
0
0
Watuhumiwa hao wakiwa mahakamani.
Raia wawili wa China walioachiwa huru wiki iliyopita katika kesi ya uvuvi haramu, wamepandishwa kizimbani tena wakikabiliwa na mashitaka ya kuvua samaki katika Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari ya Tanzania bila kibali.

Washitakiwa hao nahodha wa meli ya Tawaliq 1 iliyotumika kufanya uvuvi huo, Hsu Chin Tai na wakala wa meli hiyo, Zhao Hanquing.
Walikuwa wakitumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya uvuvi haramu.
Hata hivyo mwishoni mwa wiki Mahakama ya Rufani iliwaachia huru baada ya kushinda rufaa yao ya kupinga adhabu ya kifungo hicho au kulipa faini ya Sh bilioni 20 iliyotolewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Jana washitakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema.
Wakili Mwandamizi wa Serikali, Prosper Mwangamila alidai kati ya Januari 10 na Machi 8 mwaka 2009, washitakiwa walifanya uvuvi wa samaki katika Ukanda wa kiuchumi wa bahari ya Tanzania bila kuwa na kibali.
Alidai, katika tarehe hizo, washitakiwa hao walifanya uchafuzi wa mazingira kwa kutupa uchafu unaotokana na samaki katika bahari ya Tanzania na kuchafua maji.
Aliendelea kudai katika mashitaka mengine, kati ya Machi 8 na 11 mwaka 2009 katika eneo la Mombasa na Bandari ya Dar es Salaam Temeke, huku akijua Tai amefanya kosa la kuvua samaki bila kibali, Hanquing alijaribu kumtorosha akwepe mashitaka pamoja na adhabu.
Washitakiwa waliokuwa wakitafsiriwa na mkalimani Simon Bulenganije, hawakuruhusiwa kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa wataruhusiwa kujibu katika Mahakama Kuu.
Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na washitakiwa walirudishwa rumande hadi Aprili 14 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Machi 28 mwaka huu Mahakama ya Rufaa iliwaachia huru raia hao waliokuwa wakitumikia kifungo hicho jela kutokana na dosari za kisheria katika taratibu za kuwafungulia mashitaka kwa kuwa walifunguliwa mashitaka bila kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Washitakiwa walikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa Februari 23 mwaka juzi, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliyowapa adhabu hiyo au kulipa faini ya Sh bilioni 20 na na meli waliyokuwa wakitumia ilitaifishwa.
Awali walikuwa wakikabiliwa na mashitaka mawili ya kufanya shughuli za uvuvi katika ukanda huo wa Tanzania bila kuwa na kibali na pia kuchafua mazingira ya bahari kwa kumwaga mafuta machafu na uchafu wa samaki. Walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh bilioni.
Awali, walishitakiwa 35 ambao walitoka katika mataifa tofauti ya Bara la Asia, kama vile China, Ufilipino Vietnam na wawili raia wa Kenya, raia mmoja wa Kenya alifariki dunia akiwa mahabusu kabla kesi haijaisha. Washitakiwa 33 waliachiwa huru na wawili kutiwa hatiani
Walikamatwa Machi 8, 2009 wakati Dk John Magufuli akiwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Wanadaiwa walikutwa na tani 293 za aina mbalimbali za samaki, waliodaiwa kuwavua katika eneo la Bahari Kuu la Tanzania.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

Trending Articles