Mahakama ya hakimu mkazi mjini Moshi jana imelazimika kuahirisha kesi ya utoroshwaji wa Twiga kwenda Uarabuni baada ya hakimu mkazi Simon Kobelo anayesikiliza kesi hiyo kukabiliwa na majukumu mengine katika mahakama kuu kanda ya Moshi.
Akiahirisha kesi hiyo Hakimu Kobelo alisema ameshindwa kushughulikia kesi nyingine, ikiwa ni baada ya kuwa na majukumu mengine muhimu katika mahakama kuu na kuwa kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Machi 24 na 25, mwaka huu.
Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea kusikilizwa leo kwa upande wa mashtaka kuleta mashahidi wake wengine 39 waliobaki, ikiwa ni baada ya 21 kuwa tayari wamewasilisha ushahidi wao mahakamani hapo.
Kesi hiyo inawakabili washtakiwa wanne akiwemo raia wa Pakistan, Kamran Ahmed, Hawa Mang'unyuka, Martin Kimath na Michael Mrutu ambao wote wako nje kwa dhamana.