Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kupambana na ujangili nchini kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa.
Imeandaa mkutano wa kuwezesha utekelezaji wa shughuli za kuzuia ujangili na kupiga marufuku biashara ya vifaa vinavyotengenezwa kwa meno ya tembo halali na haramu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema hayo jana wakati akizungumzia mkutano wa wadau wa ndani na nje ya nchi kuhusu kukabiliana na vitendo vya ujangili, utakaofanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.
“Kumekuwa na mila potofu ya meno kutumika kama dawa, jambo ambalo siyo la kweli na tutapambana popote kuhakikisha tunadhibiti matumizi hayo," alisema Nyalandu.
Nyalandu alisema mkutano huo, ulioandaliwa na serikali kwa kushirikiana na na asasi ya International Conservation Caucus Foundation (ICCF) ya Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), utahusisha wakuu wa masuala ya uhifadhi, mawaziri na watendaji wengine wa kukabiliana na vitendo hivyo.
Nyalandu alisema katika mkutano huo wa kipekee Tanzania itafahamisha umma wa kimataifa namna ilivyojipanga kukabili ujangili na kuendeleza uhifadhi wa rasilimali hii muhimu kwa maisha ya watanzania na jamii ya kimataifa.
“Hivyo wadau wa uhifadhi duniani watapata fursa ya kushiriki na kuunga mkono jitihada hizo katika mkutano huo utakaofanyika kuanzia Mei 9 hadi 10 mwaka huu,”alisema Nyalandu
Alisema mkutano huo umeandaliwa kutokana na juhudi za serikali kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za taifa 16, mapori ya akiba 28, hifadhi ya ngorongoro, mapori tengefu 44, maeneo ya jumuiya ya hifadhi za wanyamapori 38 na hifadhi za misitu.
Alisema kwa mujibu wa Taarifa ya Ushindani Duniani ya mwaka 2011 Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa ubora wa maliasili baada ya Brazil.