Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

JAJI WARIOBA AWACHANGANYA WAJUMBE BUNGE LA KATIBA...

$
0
0
Jaji Joseph Warioba.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamekiri kuchanganywa kutokana na hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ambayo walidai imeibua mambo mengi ambayo hawakuwa wanayafahamu.

"Hii hotuba imeibua mambo magumu na yametikisa Muungano, mengine sikuwahi kuyasikia tangu niingie kwenye siasa," alisema Mbunge wa Kisarawe, Selemani
Jaffo.
Alisema kupitia hotuba ya Warioba, amegundua  wananchi wa pande mbili wana tofauti kubwa ya mtazamo wa Muungano uliopo, jambo ambalo alisema
linapaswa kutafutiwa dawa.
Jaffo alisema kinachosikitisha zaidi ni kwa Zanzibar kuvunja katiba na kuwa na Serikali iliyo kamili, jambo ambalo alisema limechangia kutikisa Muungano uliopo, kwani upande mmoja umevunja Katiba zaidi.
Alisema Taifa limetikisika kwa hotuba ile, lakini akalaumu viongozi ndio wameifikisha nchi hapo ilipo, kwani walishindwa kushughulikia matatizo hayo.
"Nawaasa wajumbe wenzangu tuangalie maslahi ya Taifa kwanza."
Vuai Ali Vuai ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, alisema jambo kubwa ambalo wajumbe wanatakiwa kujadili kwa kina ni muundo wa serikali tatu ambao uko kwenye rasimu na kujadili matatizo aliyoyataja mzee Warioba.
Alisema ni kweli kuna changamoto nyingi katika muundo uliopo na akasema ndio maana wajumbe wako kwenye Bunge hilo kujadili ni Katiba gani inaifaa Tanzania kwa kipindi hiki.
"Wajumbe tunatakiwa kutulia kwanza, hizi sababu alizozitaja Jaji Warioba kuna za msingi na zingine hazina msingi, hivyo ni mambo yanayohitaji tafakuri ya hali ya juu," alisema Vuai.
Alisema anaamini kwamba hekima, busara  za wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wataandika Katiba ambayo italinda zaidi Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.
Mjumbe Paul Kimiti katika maoni yake alisema Warioba alijitahidi kueleza ukweli bila kuficha, hivyo ni jukumu la wajumbe kutafakari kwa kina na kutoa michango inayoboresha zaidi rasimu ya Katiba iliyopo.
Kimiti aliwataka wajumbe waeleze faida na hasara ya serikali zinazopendekezwa na Tume  na akafafanua kuwa suala la serikali tatu ilipaswa kuitisha kura ya maoni kabla ya kuanza mchakato wa mabadiliko ya Katiba.
"Namfahamu Warioba ni mkweli na amesema anachokiamini, badala ya kuweka misimamo ya vyama tutangulize maslahi ya Taifa kwanza.
"Unajua Mzee Nyerere (Julius) alitaka serikali moja lakini hilo tumeambiwa hapa kwamba haliwezekani kwani mambo ya Muungano yanaenda yakipunguzwa kila
kukicha, miaka 50 tumevumiliana sana ni lazima tufafute suluhisho," alisema mwanasiasa huyo mkongwe.
Alitoa mwito wajumbe waache siasa badala yake watafute muafaka wa matatizo yaliyopo, ili Katiba iimarishe zaidi Muungano kwani kwenda kwenye serikali
tatu kuna athari kubwa kiuchumi na kiulinzi, na kuendelea na serikali mbili ni ngumu kwa vile kuna nchi tayari imevunja Katiba.
Innocent Kalageris ambaye ni mbunge Morogoro Kusini alisema, "Jambo hili linaumiza sana, hivi viongozi wetu walikuwa wapi akiwemo mzee Warioba mwenyewe hadi mambo haya magumu yanajitokeza hadi kutishia Muungano wetu?
"Lazima Wazanzibari wabadilishe Katiba yao, maana kule kwenye chama wanaonesha kuungana na msimamo wa CCM, iweje wasiibadili?” alihoji na kusisitiza kuwa hakuna jinsi ya kutatua suala hilo zaidi ya Zanzibar
kubadili Katiba yake.
Naye Charles Mwijage katika maoni yake aliishambulia Zanzibar kuwa walitunga Katiba ile wakati Bunge la Muungano limevunjwa na wakaingiza mambo ambayo
hayakubaliki katika muundo wa serikali mbili.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles