![]() |
Angella Kairuki. |
Kairuki aliteuliwa pamoja na Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Bongo5, Luca Nengesti.
Watanzania hao wawili wameingia katika jopo hilo, linaloundwa na vijana 214, ambapo kati yao 109 ni wanawake. Wanatoka nchi 66 duniani huku Afrika ikiwa na wawakilishi 19 pekee.
Imeelezwa kuwa nusu ya vijana hao, wanatoka katika taasisi za serikali na iliyobaki ni wa sekta binafsi.
Walipatikana kutokana na maombi ya watu 5,000, waliopendekezwa duniani kote na baadaye kufanyiwa mchujo, uliofanywa na kamati maalum chini ya uenyekiti wa Malkia wa Jordan.
Vijana hao ni vijana wenye umri chini ya miaka 40, waliosifika kwa mchango wao katika jamii.
Madhumuni ya kikundi hicho ni kuongeza ubora na uwajibikaji kwa viongozi vijana Afrika na kwingineko.
Watanzania wengine waliowahi kuteuliwa kwenye jopo hilo ni January Makamba, Mohammed Dewji, Elsie Kanza, Lawrence Masha na Susan Mashibe.