Watu wanne wameuawa na kundi la watu wasiojulikana, wakituhumiwa kuiba ng’ombe katika Kijiji cha Igwambiti Kata ya Buhongwa, jijini Mwanza.
Mtendaji wa Kata ya Buhongwa, Benedict Kabadi alisema alipokea taarifa za kuwepo kwa mauaji hayo jana asubuhi na kwamba alipofika katika eneo la tukio, aliikuta miili ya watu watatu waliouawa.
Alidai wananchi walimkamata Joseph Mwita na kumtaka awaoneshe watu anaoshirikiana nao katika wizi. Inadaiwa aliwapeleka hadi Kijiji cha Igwambiti, Kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana na kuwaonesha.
Kabadi alisema watuhumiwa hao waliuawa na kundi la watu, lakini wakati anawasili eneo hilo walikuwa tayari wametawanyika na kuacha miili hiyo.
Waliouawa ni Ezekiel Lucas (27), Kusekwa Lucas (25), Masumbuko Kisinza (30) wote wakazi wa Kijiji cha Igwambiti, Kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana na mfanyabiashara ya nyama wa Buhongwa, Mafisi Mwita (30).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola alisema watu watatu wanashikiliwa na jeshi hilo, wakidaiwa kukutwa na marungu yaliyokuwa na damu.
Alisema tukio hilo ni la jana saa 11.30 alfajiri katika Kijiji cha Igwambiti, Kata ya Buhongwa. Alisema wizi wa ng’ombe ulitokea katika Kitongoji cha Nyang’omango Kijiji cha Mtende, Tarafa ya Usagari, Wilaya ya Misungwi mkoani hapa.
Kamanda Mlowola alisema uchunguzi juu ya tukio hilo, unaendelea ili kubaini wote waliohusika kwenye mauaji hayo.