Habari zilizotufikia, zinasema kwamba timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kuibana timu ya Taifa ya Namibia na kwenda nayo sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kalenda ya FIFA uliochezwa mjini Windhoek, Namibia muda mfupi uliopita.
Taifa Stars iliyokuwa ikicheza kwa mara ya kwanza tangu kusitishwa kwa mkataba wa aliyekuwa Kocha Mkuu, Kim Poulsen, ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 89 baada ya mchezaji mmoja wa Namibia kujifunga katika harakati za kuokoa.
Lakini ukosefu wa umakini kwa mabeki wa Taifa Stars uliwagharimu dakika moja baadaye, kwa kushindwa kuwadhibiti washambuliaji wa Namibia na kufanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 90.