![]() |
Athari za mvua inayoendelea kunyesha. |
Hadhari hiyo iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Agnes Kijazi kuwa tahadhari hiyo inaanzia Machi 5 hadi kesho.
Alisema maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni ukanda wote wa Pwani katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.
Dk Kijazi alisema hali hiyo inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hewa Mashariki mwa Bahari ya Hindi na kusogea kwa haraka kwa mfumo wa mvua za msimu (ITCZ).
“Hivyo kuongeza kiwango cha unyevunyevu kutoka baharini kuelekea maeneo tajwa hapo juu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
TMA inatoa angalizo kwa wakazi na watumiaji wa bahari na mamlaka zinazohusika na maafa, kuchukua hadhari stahiki.
Alisema mvua zinazoendelea na zinazotarajiwa kunyesha, zinaashiria kuanza mapema kwa mvua za masika katika baadhi ya maeneo ya pwani ya Kaskazini, ikiwemo Dar es Salaam.
Alisema mamlaka hiyo inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi.