Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4542

PROFESA LIPUMBA AMPIGIA DEBE SITTA UENYEKITI BUNGE LA KATIBA...

$
0
0
Profesa Ibrahim Lipumba.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba, amesema Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta, ana sifa zote za kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba.

Lipumba ambaye ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, alitoa kauli hiyo  wakati akichangia hoja iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni za Bunge hilo, Profesa Costa Mahalu, kuhusu namna ya kuwasilisha maoni ya walio wachache mara vikao vya kamati vinapomalizika.
Katika mchango wake, Profesa Lipumba alisema utaratibu ambao ulitolewa na Profesa Mahalu wa kumpa Mwenyekiti wa Kamati, kuwasilisha maoni ya Kamati ya walio wengi saa moja yakiwemo na machache ya walio wachache na baadaye kumpa mjumbe wa walio wachache kutumia nusu saa kuwasilisha maoni yao,  yana mashiko.
“Kwa vile tutakuwa na mwenyekiti mwenye viwango na spidi ni wazi kuwa suala hili limekaa vizuri na naamini kuwa tutafikia suluhisho zuri,”alisema Lipumba na kusababisha makofi kutoka kwa wabunge wa bunge hilo.
Sitta ni mgombea pekee aliyepitishwa na chama chake cha CCM, kuwa mgombea wa nafasi hiyo.
Hoja ya namna ya maoni ya walio wachache yatakavyowasilishwa bungeni, juzi ilishindwa kupata ufumbuzi kutokana na mabadiliko yaliyofanywa na kamati ya kanuni kupata upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya wabunge.

Katika marekebisho ya kamati, ilipendekezwa kuwa taarifa ya kamati inayoungwa mkono na wajumbe walio wengi, itawasilishwa kwenye Bunge Maalum na mwenyekiti wa kikao cha wenyeviti au mwenyekiti wa kamati yoyote, atakayeteuliwa kwa madhumuni hayo na atawasilisha kwa saa mbili.
Katika marekebisho hayo, ilielezwa kuwa baada ya taarifa hiyo chini ya fasihi ya tisa kuwasilishwa mjumbe aliyeteuliwa kuwasilisha sehemu ya taarifa ya maoni ya walio wachache, atawasilisha taarifa hiyo kwa saa mbili.
Wajumbe walipinga marekebisho hayo na wakapendekeza kuwa wenyeviti wote wa kamati 12, kila mmoja atapewa saa moja kuwasilisha maoni ya walio wengi, jambo ambalo liliafikiwa na Bunge lote. Lakini kipengele cha namna gani maoni ya walio wachache, yatawasilishwa bungeni, yalileta kizaazaa.
Wakati wajumbe wengi wakitaka maoni ya walio wachache wasiwasilishwe bungeni, bali wachache hao wapewe nafasi ya kuchangia hoja kwa kusema maoni hayo, suala hilo lilipata upinzani kutoka kwa makundi mbalimbali, vikiwemo vyama vya siasa hasa wabunge wa upinzani.
Tundu Lissu ambaye alikuwa anafafanua hoja hizo kwa wajumbe, alisimama kidete kuliambia Bunge hilo kuwa kamwe hawatakubali maoni ya wachache, yasiwasilishwe bungeni na akasisitiza kuwa maoni hayo ni lazima yawasilishwe, jambo ambalo lilileta sintofahamu hadi Bunge likaahirishwa juzi.
Jana, Profesa Mahalu na kamati yake walilazimika kuliambia Bunge kuwa kutokana na mvutano uliojitokeza juzi, wamelifanyia mabadiliko suala hilo kwamba sasa taarifa ya walio wachache, itasomwa bungeni kwa nusu saa baada ya mwenyekiti wa kamati husika kuwasilisha maoni ya walio wengi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4542

Trending Articles