![]() |
Bernard Membe. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amepongeza hatua ya CCM kumpa onyo kali na kumweka chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, kutokana na kubainika kuanza kampeni za urais kabla ya muda.
Membe aliyeelezea sababu za kutokea kwa utovu huo wa nidhamu, amesifu utaratibu huo wa CCM kuadhibu makada wake kuwa ni sahihi na mfumo mzuri wa kutengeneza nidhamu ndani ya chama.
Membe alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya utekelezaji ya Wizara hiyo kwa mwaka 2013.
“Ukiona chama hakina utaratibu wa kuratibu, kujisimamia na kuweka nidhamu, ujue hakina faida ya kuwapo. Nasisitiza kuwa taratibu hizo ni za kawaida na za lazima hasa kwa watu waliooteshwa na wasiooteshwa kama mimi,” alisema Membe.
Membe na makada wengine watano wa chama hicho, wanatuhumiwa kuanza kampeni mapema za urais kinyume cha utaratibu na mwongozo wake.
Makada wengine ni waliopata kuwa mawaziri wakuu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba.
Wote waliitwa Dodoma na kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kuhusu madai ya kuanza kampeni mapema zinazodaiwa kuivuruga CCM na wanachama wake.
Baada ya kumaliza kuwahoji Jumapili iliyopita, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alitangaza Dar es Salaam adhabu hiyo.
Nape alisema baada ya kuwahoji, walithibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea urais kabla ya wakati, jambo ambalo ni kinyume cha Kanuni za Uongozi na Maadili ya CCM.
Membe alisema fujo na vurugu zinazotokea wakati uchaguzi ukikaribia, katika nchi nyingi duniani ikiwamoTanzania, kutokana na kushindwa kufuata mfumo wa kupata kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani nchini Vatican.
Alisema mfumo huo wa kumpata Papa ni bora kwa kuwa hauna makundi, kampeni wala kuhamasisha achaguliwe nani, bali kiongozi atakayepata kura nyingi za makadinali ndiye hutangazwa na kushangiliwa kwa kishindo duniani kote.
“Ndiyo maana vyama vya siasa vina changamoto ya kupata kiongozi bora, kutokana na hilo, vina wajibu mzuri wa kuratibu namna nzuri ya kupata viongozi hao,” alisisitiza.
Alisema utaratibu wa adhabu uliotumiwa na CCM ni mzuri kwa kuwa chama hicho bado hakina utaratibu wa kupata kiongozi unaotumiwa na Vatican.
Membe alisema katika kuchagua kiongozi, Wakatoliki wamekuwa wakitumia njia bora ya kukutanisha makadinali wote duniani katika nyumba moja inayoitwa Basilika, ambako husali na kupiga kura ya kuchagua kiongozi wanayeona anafaa.
“Wamejiwekea utaratibu wa kuchagua kiongozi wao ambao dunia nzima imeshindwa kuuiga, mambo mengine yote tumewaiga, mavazi ya madiwani, mavazi ya wahitimu katika mahafali, mavazi ya majaji, yote haya ni utamaduni wa Wakatoliki, lakini hili la uchaguzi wa kiongozi tumeshindwa,” alisisitiza.
Alisema kutokana na ukweli kuwa nchi nyingi duniani ikiwamo Tanzania zimeshindwa kufuata mfumo mzuri wa kutafuta kiongozi kama ulivyo mfumo wa Vatican, vyama vya siasa havina budi kujiwekea utaratibu wa kupata kiongozi bora na kulinda nidhamu.